Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre)
Brigedia Jenerali Anselim akiongea na waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo
inayodhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa
matrekta madogo( power Tiller) ambayo yanalenga kumkomboa mkulima hapa
nchini kwa kuondokana na matumizi ya jembe la makono.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali
Anselim.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe akiongea na Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutoa habari za kuelimisha kwa jamii
hasa zitakazowawezesha kuwajengea uwezo wa kimaarifa na kuwainua kichumi
kupitia elimu hiyo.
Mhandisi
Mkuu Msanifu Albert Wikedzi akiwaonesha waandishi wa Habari (Hawapo
pichani) aina mbalimbali za sanifu zinazofanyika katika shirika hilo,
wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda hicho Mjini kibaha.
Mkuu
wa Kitengo cha Usubiaji Mhandisi Anderson Ole Zakaria akiwaeleza
waandishi wa habari namna kitengo hicho kinavyofanya kazi ili kukidhi
mahitaji ya kiwanda ambapo alisema kitengo hicho kinayeyusha hadi tani
2.5 za chuma zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotoka
katika shirika hilo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre)
Brigedia Jenerali Anselim akiwaonesha waandishi wa habari moja aina ya
gari la kivita lililotengezezwa na shirika hilo.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni