Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka
kwenye Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez
Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika Agosti 6, 2015
jijini Ismailia. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana
ameiwakilisha Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha
mabara ya Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita "zawadi
mpya kwa Dunia" unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na
utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri ambayo
kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana na meli
zitakazopita katika mfereji huo.
Mradi
wa ujenzi wa Mfereji huu mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa
kukamilika baada ya miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni
Nane ambazo zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi
kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa kwa
Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli kusimama ili
kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila kuathiri upande
mwingine.
Sherehe
hizo za aina yake zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata
kuripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika
inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa fursa
mpya za maendeleo zipo Afrika.
Sherehe
hizo za aina yake zilipambwa na maonesho
ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji mpya wa Suez huku zingine
zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi bendera ya Misri, zingine
zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.
Katika
tukio
hilo la kuathimisha tukio hilo la kihistoria serikali ya Misri
ilitangaza kuwa siku hiyo ni ya mapumziko huku ulinzi mkali
ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya nchi hiyo huku jiji la Cairo
walipofikia viongozi mbalimbali wa kimataifa likiwa chini
ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote muhimu. Barabara ya kwenda
eneo la
Islamelia zilikofanyika sherehe hizo ilifungwa kwa siku nzima,
walioruhusiwa kupita ni viongiozi na wageni mbalimbali waalikwa
waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la
kihistoria.
Rais wa Misri Abdel Fatah Sisi alisema kufunguliwa kwa Mfereji ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na kueleza
kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na kufungua fursa
zaidi kwa mataifa duniani.
Katika
moja ya matukio ya uzinduzi huo Rais
Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo walisafiri katika meli
za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri akivalia mavazi maalumu ya kijeshi
akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa
miaka tisa aliyevalia kijeshi na kupeperusha bendera ya Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa
mfereji huo.
Shughuli ilimazika usiku kwa maonesho
mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri
na kuhudhuriwa na viongozi na wageni wote waalikwa.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
Cairo
Misri Agosti 7, 2015
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni