Mratibu
wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Dkt. Upendo Mwingira, akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa
uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa
mabusha Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika
hospitali ya Mkoa ya Ligula.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) na Mwenyekiti wa
magonjwa yasiyopewa kipaumbele Afrika Dkt. Mwele Malecela akitoa salamu
kwenye uzinduzi wa kambi hiyo, ambapo alisema Matende na mabusha ni
magonjwa ambayo yanatakiwa kutokomezwa ifikapo mwaka 2020 nchini
Tanzania.
Mkurugenzi
wa Idara ya Kinga ,wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema
Rusibimayila, akipokea mfano wa hundi toka kwa mwakilishi wa Stat Oil
Naomi Makota (kulia) kwa ajili ya upasuaji wa wagonjwa wapatao 100 wa
Manispaa ya Mtwara.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kambi
hiyo ya upasuaji Johansen Bukweri akizungumza kwenye uzinduzi huo,
alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakiathiri
sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wa Mtwara na kuleta mahangaiko mengi
kwa wananchi ikiwemo ulemavu, hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi
kushiriki katika ujenzi wa Taifa na watoto kutoweza kuhudhuria vizuri
katika masomo shuleni.
Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
Dkt.
Upendo Mwingira akiwafariji wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa
mabusha katika hospitali ya mkoa ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5.
Mkoa wa Mtwara una takribani watu wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na
ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika kwa watu waliojiandikisha na
itatolewa bila ya malipo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni