Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma 
Na Mwandishi wetu,Arusha
Mkuu
 wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika 
tamasha la 10 la vyombo vya habari  vya mkoa wa Arusha. ambalo 
litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Akizungumza
 na waandishi wa habari Palace hoteli jana  mwenyekiti wa TASWA mkoa wa 
Arusha, Jamila Omar  na Katibu wa TASWA Arusha,  Mussa Juma walisema 
maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka
 jijini Dar es Salaam. 
Omar
 alisema Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo ni kuwa,Uchaguzi bila 
vurugu inawezekana na   timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio 
zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira wa pete.
 
Alisema
 mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo 
wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T) 
Ltd. 
Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
 
Akizungumzia
 tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka 
wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL 
itaendelea kushirikiana na wanahabari.
Awali
 Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine 
zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio 
,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
 
 Alisema kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea hifadhi
 ya Taifa ya Arusha vile vile  kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa 
Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi  mkoani hapa ikiwa ni sehemu 
ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo 
 
 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni