wanaapolo wakiwa mgodini (picha na maktana)
Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
Wachimbaji wadogo wawili (wanaapolo) wanaofiwa kufa na wengine kadhaa
kujeruliwa katika mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Mererani
mkoani Manyara .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia leo ambapo wachimbaji hao
waliangukiwa na kiberenge ndani ya mgodi huo uliopo block C unao
milikiwa na Said Nassor (mwarabu) walipo kuwa wakiendelea na kazi.
Shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edison Onyango alisema kuwa
kiberenge hicho kilikatika na kuporomoka na kisha kuwaangukia watu hao
na kusababisha vifo na majeruhi.
Akizungumza kwa njia ya simu mmiliki wa mgodi huo Said Nassor
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wamepata maiti ya
mtu mmoja na wako katika harakati za kusafirisha mwili huo kwenda kwa
ndugu zao kwa ajili ya maziko.
Hata hivyo alieleza kuwa tukio hilo ni lakawaida na kwamba polisi
walifika kwa ajili ya uchunguzi wakiwemo maofisa wa idara ya madini
ili kuchunguza undani wa tukio hilo.
www.woindeshizza.blogspot.com
“kwakweli ndugu muandishi wa habari tukio hili ni kweli limetokea
katika mgodi wangu na alijasababishwa na uzembe ila ni tukio la
kawaida kutokea na linaweza kutokea katika mgodi wowote “alisema Said
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa aliyefariki dunia
ni mtu mmoja Joseph Kimati (27).
Aliongeza kuwa waliojeruliwa katika tukio hilo ni wawili ambao
aliwataja kwa majina ya Regan Rabiel(29) na Hussen Juma (25)na kueleza
kuwa chanzo cha tukio ni kiberenge kilichokatika na kupoteza
muhelekeo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni