Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akiwa
anamkabidhi kikombe Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya mara
baada yakituo cha Radio5 kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa
Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha
sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya
Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa ameshikilia kikombe walichoshinda katika maonyesho ya nanenane
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya akiwa na timu yake ya ushindi mara baada ya kituo hicho kutangazwa
washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya
mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na
maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa
maonyeshoThemi Mkoani Arusha
Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya
wa Radio 5 akiwa anamkabidhi funguo ya pikipiki kwa Mkuu wa wilaya
Monduli Jowika Kasunga zawadi ya mshindi wa kwanza katika kilimo
Kushoto
ni Rais wa Taasisi ya upendo kwa mama Eng.Carlos Mkundi akiwa katika
banda la Radio 5 na DJ Haazu ambapo Taasisi ya upendo kwa mama
wamedhamini maonyesho ya nanenane kupitia kituo cha Radio 5
Wafanyakazi wa Radio 5 katika nyuso za furaha
Kituo
cha Radio 5 kilichopo jijini Arusha kimeshika nafasi ya kwanza katika
maonyesho ya nanenane kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima
ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane
na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja
wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
Akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu Meneja masoko na mawasiliano
Sarah Lazaro Keiya alisema kuwa wanafuraha kubwa kwa kupata ushindi huo
Pia Radio hiyo imekuwa ikiwapatia wakulima msaada wa mbegu,mbole na wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kujua maendeleo yao katika masuala ya kilimo
“Vipindi vyetu vya kilimo vimekuwa vikitupa tuzo mbalimbali nah ii leo katika maonyesho haya pia tumepata tuzo”alisema Keiya
Aidha alisema kuwa wamekuwa wakitoa zawadi kila mwaka kwa mkulima bora atakayechaguliwa na TASO ambapo wametoa pikipiki aina ya powew king yenye thamani ya shilingi milioni mbili,mbole pamoja na mbegu
Hata hivyo alitoa shukrani zake kwa mkurugenzi wa kituo hicho Bw,Robert Francis kwa kuwawezesha wafanyakazi kufanya vizuri katika maonyesho hayo huku akisema kuwa anatimu nzuri inayojituma na yenye uwezo mkubwa kikazi
Aliwashukuru wadhamini SBs(pepsi),Kishen
enterprises limited,Upendo kwa mama foundation,Grandmaster records,Atown
records na wote waliojitokeza kushirikiana nao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni