Liverpool imekwea kileleni mwa Ligi
Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza ikinolewa na kocha Jurgen Klopp
kwa kupata ushindi mnono wa magoli 6-1 dhidi ya Watford katika dimba
la Anfield.
Sadio Mane aliifanya Liverpool
iongoze kwa kufunga kwa mpira wa kichwa cha sarakasi, baada ya
wenyeji hao kukosa nafasi kadhaa, na kisha baadaye Philippe Coutinho
kufunga la pili kwa shuti la umbali wa yadi 20.
Adam Lallana alimdondoshea krosi
Emre Can na kufunga goli la tatu kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili
kilipoanza Roberto Firmino aliunganisha kimiani pande la Lallana
kabla ya Mbrazili huyo kumtengenezea goli Mane na kisha Georginio
Wijnaldum kutikisa la sita.
Msenegal Sadio Mane akiruka kichwa cha sarakasi na kufunga goli la kwanza
Roberto Firmino akiifungia Liverpool goli la nne katika mchezo huo
Sadio Mane akifunga goli lake la pili katika mchezo huo ambalo lilifikisha idadi ya magoli matano ya Liverpool
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni