Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Urio
akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Chakuwama kilichopo Sinza wakati wa hafla fupi ya kutoa msaada iliyofanyika Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Kituo hicho, Hassan Hamisi (kulia), akitoa historia fupi ya kituo hicho.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakiwa wamewabeba watoto katika hafla hiyo.
Mfanyakazi bora wa benki hiyo, kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba, Amani Mgweno akishiriki kubeba zawadi za watoto hao.
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kushoto), akishiriki kutelemsha zawadi hizo kutoka kwenye gari.
Zawadi zikiendelea kutelemshwa.
Zawadi zikitelemshwa. Kulia ni mtoto wa
mfanyakzi wa benki hiyo, Asha Mayuva, akionesha upendo kwa watoto
wenzake kwa kuwapelekea zawadi.
Wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa wamewabeba watoto mapacha wanaolelewa katika kituo hicho.
Zawadi zikipangwa. Kutoka kushoto ni
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio, Asha Mayuva, Raphael Mlute na Magreth
Lwiva. ' Hapa ni Kazi Tu kwa kwenda'
Taswira ya keki maalumu kwa ajili ya
watoto hao ' Hakika NMB Tawi la Mlimani City mmeonesha upendo wa hali ya
juu kwa watoto hao barikiweni sanaaa'
Mwonekano wa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na watoto hao.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa kwenye hafla hiyo fupi.
Hapa ni furaha tupu.
Hapa ni nani kama baba?
Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ikikatwa.
Hapa ndipo unapoweza kuutambua utamu wa keki.
"Hapa ni kama wanafikiria sijui tuondoke na mtoto huyu"
Na Dotto Mwaibale
BENKI ya NMB Tawi la Mlimani City imetoa
msaada wa vitu mbalimbali kwa Makao ya Kulea Watoto Yatima ya
Chakuwama yaliyopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya njia ya
kujumuika na jamii inayo wazunguka.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi
katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo ambao ni vyakula na vifaa vya
shule kwa ajili ya wanafunzi Meneja wa benki hiyo wa tawi hilo, Seka
Urio alisema ni kawaida kwa benki hiyo kushiriki shughuli za kijamii na
kutoa faida wanayoipata kwa wananchi ambao ndio wateja wao.
"Tunajisikia faraja kutoa vitu vichache
kwa watoto wetu ambao mnawalea katika kituo hiki pia ni kurudisha faida
tunayoipata kwa jamii" alisema Urio.
Urio alisema vitabu vyote vya dini vinaelekeza kuwajali na kuwafariji wenzetu wenye uhitaji ikiwa ni agizo lake mwenyezi mungu.
Katibu wa Kituo hicho, Hassan Hamisi
alisema kituo hicho chenye watoto 60,000 wakike wakiwa 25 na kiume 35
tangu kianzishwe kwake mwaka 1998 kimepata mafanikio ya kupata nyumba
yao ya kuishi watoto hao, malezi huduma za elimu na afya.
"Kwa kweli tukiangalia tulipoanzisha
kituo hiki na sasa tumepiga hatua licha ya kuwepo changamoto kwani
tunasomesha watoto katika shule mbalimbali za sekondari na msingi na
wengine wapo vyuo vikuu ni jambo la kujivunia" alisema Hamisi.
Alisema watoto wengine wamepata kazi
baada ya kuhitimu elimu katika ngazi mbalimbali na baadhi yao wameoa na
kuolewa na sasa wanaendesha familia zao.
Hamisi alimshukuru Rais Dk.John Magufuli
kwa kuanzisha utaratibu wa wanafunzi kupata elimu bure kwani
umewapunguzia changamoto ya kuwalipa ada wanafunzi 47 wanao walea katika
kituo hicho.
Hamisi alisema pamoja na kupiga hatua
bado wanachangamoto mbalimbali kama chakula na nyumba kwani kila siku
watoto wamekuwa wakiongeza katika kituo hicho kutokana na migogoro ya
kifamilia, wazazi au walezi kufariki na kuwaacha watoto na watoto
kutelekezwa hivyo akawaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia kama
ilivyofanya benki hiyo.
Hafla hiyo ilihudhuria na wafanyakazi wa
benki hiyo ambapo waliwafariji watoto yatima kwa kuwapa vitu mbalimbali
na kuzungumza nao ambapo waliwasisitizia kuzingatia masomo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni