Kimbunga chenye nguvu kubwa ambacho hakijawahi kutokea karibu muongo mmoja kupita kimewafanya maelfu ya watu nchini Haiti kuacha makazi yao, huku maafisa wakihaha kufikia maeneo yaliyoathirika zaidi.
Kimbunga hicho kinachoambatana na mvua kiitwacho Matthew kinasemekana kimeathiri baadhi ya maeneo ya taifa hilo la Haiti, ambapo watu wawili wameripotiwa kuwa wamekufa.
Kimbunga hicho sasa kinaelekea pwani ya kaskazini mashariki mwa Cuba, kuelekea Florida ambapo tahadhari tayari ishatolewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni