Nchi ya Haiti imeanza zoezi la kuhamisha wakazi waliopo kwenye maeneo hatarishi kutokana na kimbunga kikubwa kiambatanacho na mvua kiitwacho Matthew, kinachotisha kuleta maafa, mafuriko kikiwa na upepe wenye kasi ya kilomita 240 kwa saa.
Kimbunga hicho ni kukikubwa kulikumba eneo la Atlantic kwa karibu muungo mmoja, kinatarajia kuikumba Haiti na Jamaica hapo kesho, Kituo cha Taifa Cha Vimbunga cha Marekani kimeeleza.
Wakazi wa maeneo hatarishi wameanza kuweka akiba ya mahitaji yao muhimu, huku Waziri Mkuu wa Jamaica akiwataka wananchi kujiandaa kukabiliana na janga hilo kabla ya muda wa kufanya hivyo hauajaisha.
Watu wakifanya manunuzi ya mahitaji yao muhimu ya kutosha ili kujiwekea akiba kabla ya kimbunga Matthew hakijanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni