Nyota wa tamthilia ya maisha ya uhalisia nchini Marekani ya Keeping up with the Kardashians, Kim Kardashian, ameibiwa kwa mtutu wa bunduki kwenye chumba cha hoteli aliyofikiwa Jijini Paris nchini Ufaransa.
Mumewe mwanamuziki rapa Kanye West, alilazimika kuondoka mapema jukwaani alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la Meadows Festival Jijini New York baada ya kupata taarifa hizo za kushtua.
Msemaji wake amesema Kim Kardashian West alishikilia mtutu akiwa chumbani kwake kwenye hoteli Jijini Paris jana usiku na wanaume wawili waliojifunika sura waliokuwa wamevalia kama maafisa polisi.
Polisi Jijini Paris wamethibitisha kufanyika wizi wa kutumia silaha kwa Kim Kardashian lakini hakudhuriwa na kuongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Kanye West akitumbuiza kwenye tamasha kabla ya kuamua kuondoka jukwaani baada ya kupata taarifa za mkewe Kim kuibiwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni