MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUTATUA KERO ZA WANANCHI WILAYA YA NGORONGORO


    Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akifuatilia na kunakili hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali zinazofanya shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro wakati wa Kikao kilichofanyika katika Ofisi yake.

     Mkurugenzi wa Taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya NGO anayoiongoza wakati wa kikao maalum na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.

     Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha wakifuatilia kikao wakati wa uwasilishaji wa taarifa za Taasisi na Kampuni zisizo za Kiserikali zinazofanya kazi katika Wilaya ya Ngorongoro

   
 Wadau toka kwenye  Kampuni  na Taasisi mbalimbali kutoka Ngorongoro walioshiriki katika Kikao maalumu kilichoitihswa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha

     Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega wakati wa Kikao na NGO’S NA Kampuni zinazoendehsa shughuli zake katika Wilaya ya Ngorongoro.

 
Mkurugenzi wa taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko (kushoto) pamoja na   Manger wa Kampuni ya Thompson Safaris (kulia) kila mmoja akielezea namna ambavyo mgogoro wa ardhi uliopo unavyoathiri shughuli zao za kila siku.

Nteghenjwa Hosseah - Arusha
RC ARUSHA AKERWA NA HALI DUNI YA NGORONGORO
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo mwishoni mwa wiki hii amekutana na wadau wa taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na makampuni yanayoendesha shughuli zao katika Wilaya ya Ngorongoro lengo ikiwa ni kusikia namna wadau hao wa maendeleo wanavyoendesha shughuli zao halkadhalika  Wilaya hiyo inavyonufaika na uwepo wa wadau hao katika maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa kufungua Kikao hicho Rc Gambo alisema malego ya Kikao hiki yanaendana sambamba na maandalizi ya Safari yake ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Ngorongoro itakayoanza tarehe 03-08/10/2016 hivyo angependa kufahamu kwa upana namna ambavyo wadau hawa wanachangia katika kuleta maendeleo ya Wilaya hii ambayo kwa kipindi kirefu imekua nyumba kimaendeleo.
Alisema sielewi kwa nini kwa miaka yote hii Wilaya ya Ngorongoro haina hata kilomita moja ya barabara ya Lami, Stendi ya Kisasa wala masoko yenye hadhi ya kuwahudumia wageni ambao wengi wao ni watalaii wakati kuna taasisi za Kiserikali na siziso za Kiserikali ambazo zina uwezo wa kutosha kuboresha huduma hizi kwa manufaa ya wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.
Wananchi wa Ngorongoro wamekua na maisha duni na matatizo yasiyoisha, hakika sasa umefika wakati wa kufahamu kazi zinazotekelezwa na  kila mdau na tufahamu kwanini uwepo wao hauchangii kulete mabadiliko chanya katika Wilaya hii, huenda mipango kazi yao iko tofauti na malengo na matarajio yetu hivyo tusije tukawalaumu kumbe ni kutofahamu namna ambavyo taasisi zenu zinafanya kazi aliongeza.
“Katika Wilaya hii ukizungumzia Taasisi kubwa za Serikali kuna Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Baraza la wafugaji pamoja na Halmashauri ambao wanapata Fedha nyingi kwa ajili ya kuleta maendeleo lakin bado kasi ya maendeleo kwa kweli hairidhishi kabisa, ni vyema basi kwa pamoja tutafute majawabu ya matatizo yanayoikabili Ngorongoro”, alisema Gambo.
Baada ya Taasisi zote kuwasilisha taarifa zao iligundulika kwamba kuna mgogoro wa Ardhi ambao sasa umekua wa muda mrefu kati ya Vijiji vya Sukenya, Soitsambu, Mondorosi na Muwekezaji wa Kampuni ya Thompson.
Rc Gambo alisema ni wakati sasa wa kuketi meza moja na makundi yote kuona namna ambavyo tunaweza  kutatua mgogoro huu ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao na Muwekezaji afanye kazi zake kwa amani katika eneo hilo na kupitia kikao hiki nimepata kufahamu vitu vingi ambavyo ntakuja kuvifanyia kazi wakati wa Ziara yangu.
Ziara hii ya Kikazi Wilayani Ngorongoro itakua ya pili tangu Mhe. Gambo alipochaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema mwezi Agosti 2016.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni