…………………………………..
RAIS Jakaya Kikwete amezitaka nchi za Afrika kukumbuka
mauaji ya halaiki ya watu nchini Rwanda na kuwa mfano hai wa kukataa
matukio kama hayo kutokea katika nchi zao.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo alipokua akiweka jiwe la
msingi la ujenzi wa jengo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu katika
eneo la Laki Laki Kisongo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alisema kwa namna hali ilivyokuwatete nchini Rwanda katika
kipindi cha tukio la mauaji hayo ni kielelezo tosha cha kukataa kata
matukio kama hayo kutokea katika nchi zao kwa kuayalikuani mauaji ya
kutisha na ya kusikitisha.
Alitolea mfano wa na nchi wa Tanzania waishio katika maeneo
ya mipakani ambayo walishuhudia maelfu ya miili ya binadamu wasio na
hatia ikielea ndani ya maji ya mto Kagera ambapo hakuna aliyetamani
kuendelea kuitazama miili hiyo.
Aidha aliipongeza serikali ya Rwanda chini ya Rais wake
Paul Kagame kwa kuirejesha nchi hiyo katika hali nzuri baada ya miaka
mingi ya machafuko na kuwezesha kuurejesha uchumi mzuri kwa nchi na
wananchi wake katika kuwahakikishia usalama wao na mazingira bora ya
kujitafutia kipato.
Pia aliahidi Tanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa
uongozi wa mahakama hiyo kwa mambo mbalimbalimba liikiwemo ukamataji na
ufikishaji wa wahalifu hao katika mahakama hiyo pamoja na uwezeshaji
uliofanywa na Tanzania ikiwemo kutoa eneo la ujenzi wa mahakama hiyo
kama mchango wake.
Aliwataka wa kandarasiwa ujenzi huo kuifanyakazi yao kwa
wakati muafaka ili kuweza kuendana na kasi ya upatikanaji wa mahakama
hiyo ilishughuli hizo zianze mara moja kama hatua ya kupinga kuendelea
kutokea kwa mauaji ya namna hiyo.
Naye Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kimataifa Mahadh Juma Maalim alisema serikali ya tanzania inadhamira ya
dhati katika upatikanaji wa mahakama hiyo na ndiyo maana hadi hivi sasa
wizara yake imeshaanza ushirikiano na wizara zingine katika upatikanaji
wa miundombinu mbalimbali ikiwemo maji,umeme pamoja na mawasiliano ya
intaneti.
Aidha alisema serikali imeweza kutoa eneo la ujenzi wa
mahakama hiyo ambalo limeshapimwa na kupewa hatimiliki lenye ukubwa wa
zaidi ya hekari 16 ambazo zina amini kazi tatosheleza ujenzi huo pamoja
na miundombinu mingine mbalimbali.
Naye mkurugenzi wa maendeleo wa umoja wa mataifa na
msimamizi wa mradi huo John Hokings aliishukuru serikali ya Tanzania kwa
moyo wa dhati wa kuihitaji mahakama hiyo kwa kutoa eneo pamoja na
nguvukazi kwa ajili ya ujenzi huo.
Alisema wao kama viongozi wa umoja huo walikaa na
kutathimini na kuona ilikuonyesha shukurani kwa serikali ya Tanzania
ndipo walipoamua kuurejesha mradi huo kwa serikali hiyo katika ujenzi
wake kwa kuzikabidhi kampuni wazawa kuendesha ujenzi wake.
Ujenzi wa mahakama hiyo ulianza mnamo Desemba 22,2010,
chini ya umoja huo ilikushughulikia mauaji ya halaiki ya liyotokea
nchini Rwanda mnamo mwaka 1994 pamoja na uhalifu wa kivita popote
ulimwenguni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni