WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu, akirejesha fomu za wadhamini kwa Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara), Rajabu Luhavi, jana, baada ya kukamilisha kazi ya kuomba
udhamini kwa mikoa yote nchini.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu, akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Naibu Katibu
Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi. Kulia ni mkewe Faraja na kushoto ni Luhavi.
MKE wa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara), Rajab Luhavi ofisini kwake katika Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma, wakati Nyalandu aliporejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa
kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais.
BAADHI ya wanachama wa CCM
waliomsindikiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM mjini
Dodoma, jana.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakipongezwa na sehemu ya umati
uliojitokeza kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati
akirejesha fomu.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakishangiliwa na mamia ya wanachama
wakati wakiondoka ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, jana baada
ya kurejesha fomu za kuomba urais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni