Wafanyakazi wa Green WestPro waichangia damu Hospitali ya Muhimbili
Katika kusaidia na kuhakikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inakuwa na akiba ya kutosha ya damu, wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green WestPro kwa pamoja wamechangia damu kwa ajili ya hospitali ya Muhimbili.
Akizungumza na MO BLOG kuhusu zoezi hilo, Meneja Mwendeshaji wa Green WestPro, Abdallah Mbena alisema wameamua kuchangia damu kwani wanatambua kuwa Hosptali ya Muhimbili inakabiliwa na upungufu na damu na hivyo msaada ambao wanautoa utaweza kusaidia kuoa maisha ya watanzania ambao wanauhitaji wa damu.
"Tunafanya mambo mengi, tunashiriki shughuli nyingi za kijamii na kwasasa tunaona Muhimbili ina uhitaji mkubwa wa damu, kuna watoto wanafanyiwa upasuaji, kuna watu wanapata ajili hawa wote ni ndugu zetu na tunaona ni muhimu kusaidia kuokoa maisha yao," alisema Mbena.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Muhimbili, Erica Ishengoma alisema kwasasa hospitali ya Muhimbili imekuwa na mahitaji makubwa ya damu kutokana na kuongezeka kwa huduma kama ya upasuaji wa moyo lakini changamoto kubwa ambayo inawakabili ni upungufu wa damu.
"Mara nyingi watu hawajitokezi kutoa damu na mahitaji ni makubwa, tunafanya upasuaji wa moyo na unahitaji damu kwa kiasi kikubwa, kwa sasa tuna wastani wa kutumia chupa za damu 200 hadi 120 kwahiyo tunahitaji sana jamii ijitolee damu kuwasaidia wahitaji," alisema Erica.
Aidha aliishukuru Green WestPro kwa wafanyakazi wake kujitolea damu na kwa wote ambao wametoa damu zao kuwapatia kadi maalumu ambazo zitawawezesha ndani ya miezi mitatu tangu kutoa damu kama wakiwa na ndugu ambae atakuwa na uhitaji wa damu hospitalini basi ataweza kupata damu bure.
Meneja Mwendeshaji wa Green WestPro, Abdallah Mbena akipima uzito kabla ya kutoa damu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni