Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua Leo.
Klabu
ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama
ambazo zinamwezesha kila Mwanachama wa Simba kupata bima ya maisha
hadi Tsh 250,000 ikiwa atafiwa na mwenza au mtoto au yeye mwenyewe
kupitia bima ya maisha iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba leo hii
imezindua Kadi za watoto yaani Simba Cubs.
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto Iqram Ally Kadi ya Simba Cubs waliyoizindua leo wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange
Akizungumza
wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba
inaendeleza falsafa yetu ya utendajii kifanya kazi ‘’maneno machache
vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia
mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani
yake, leo tumewaita hapa kuandika historia mpya kwa wana Simba na
hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.
Aliongeza
kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba
anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama
kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz .
Napenda mtambue hii ni historia katika ukanda huu kuweza kutumia
teknojia kufikia wanachama, Sisi ni wakisa sana tunaona mbele!.
AfisaMtendajiMkuuwa
EAG Group Imani Kajula (Kulia) Akielezea Jambo Akiwa Ameambatana na
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Wakati wa Uzinduzi wa
Kadi Hiyo ya Simba Sport Club Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya
Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri
watekelezaji wa mikakati ya masoko na biashara Imani Kajula alisema
‘’
Uanzishwaji wa Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto sio
tukutambuliwa kuwamemba wa Simba, bali pia kupata punguzo kubwa
au kuingia bure kwenye matukio yanayo andaliwa na Simba Sports
Club. Pia maduka mbalimbali yatatoa punguzo kwa watoto wenye
Simba Cub Card.
Wote
mna jua fika kuwa mapenzi hujengwa, Simb aina lenga kujenga
msingi imara wa kuendeleza wanachama na wapenzi wake’’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni