AJALI ILIYOCHUKUA UHAI WA WATU SABA AKIWEMO MWANAHABARI WA GAZETI LA HABARI LEO.

Mkuu wa wilaya ya Rombo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Rombo,Agnes Hokororo akizungumzia tukio la jali hiyo.
 Na Mahmoud Ahmad kilimanjaro.

Watu saba wamekufa papo hapo katika ajali iliyotokea eneo la Mwika Mawanjeni maarufu kama 'Baa Mpya' akiwemo mwanahabari wa magazeti ya serikali na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai,Arnold Swai.

Swai na wenzake walikuwa wakitokea katika sherehe ya miaka 40 ya CCM ambayo kwa mkoa wa Kilimanjaro ilifanyika pia wilayani Rombo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo alisema ajali hiyo ikitokea majira ya saa 12 jioni katika eneo hilo na kuhusisha magari mawili pamoja na pikipiki moja.

Wengine waliifariki katika ajali hiyo ni pamoja na Anastazia Malaysia ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (Mocu) na mkazi wa Shimbi, Rombo, na Edwin Msele, katibu wa hamasa Shirikisho la vyuo vikuu Moshi mjini.

Wengine ni Ally Mbaga (Mjumbe wa NEC) wilaya ya Same na mkazi wa Mwanga, mwanamke ambaye jina halijatambulika aliyekuwa kwenye gari la Fuso, mkazi wa Himo, mwanamke aliyekuwa kwenye bodaboda ambaye fuso liligonga pikipiki hiyo na mtu mwingine mmoja ambaye hajafahamika.

Hokororo alisema majeruhi ni mwanahabari Jackson Kimambo aliyekuwa dereva wa Toyota surf hali yake inaendelea vizuri akipata matibabu hosptali ya rufaa ya KCMC.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospital hiyo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni kuwa gari la Fuso lilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro anatarajia kukutana na waandishi wa habari kuzungumzia tukio hilo.

Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni