BONDIA CHRIS EUBANK JR ATWAA UBINGWA WA IBO SUPER MIDDLEWEIGHT


Bondia Chris Eubank Jr ameshinda mkanda wa IBO wa super middleweight kufuatia ushindi alioupata katika raundi ya 10 dhidi ya Renold Quinlan wa Australia.

Eubank Jr mtoto wa bondia wa zamani wa Uingereza, amepata ushindi wake katika raundi ya 10 kwa ngumi kali ya kidevu katika mchezo uliofanyika Kensington Olympia, London.

Refa Howard Foster aliingilia kati kumaliza mchezo huo, na Eubank Jr kupatiwa mkanda wa IBO super middleweight.
                                            Chris Eubank Jr akimshindilia ngumi Renold Quinlan
     Chris Eubank Jr akiwa amemtupia konde zito lililomuingia barabara Renold Quinlan
   Chris Eubank akiwa amevaa mkanda alioutwa kulia mwenye bendera baba yake bondia maarufu wa zamani Eubank 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni