SERIKALI YA KASHMIR YAPIGA MARUFUKU HARUSI ZA MATANUZI



Serikali ya India inayoongozwa na Kashmir imepiga marufuku harusi za gharama kubwa katika eneo hilo.

Sherehe ya upande wa bibi harusi hairuhusiwi kualika watu zaidi ya 500, na kwa upande wa bwana harusi sherehe yao hairuhusiwi kualika watu zaidi ya 400.

Serikali ya Kashmir pia imesema mlo katika harusi haupaswi kuzidi vyakula vya aina saba, ili kuhakikisha kuwa hakuna chakula kinachopotezwa.

Aidha, mbunge mmoja anapanga kuwasilisha pendekezo kama hilo ili kudhibiti harusi za gharama kubwa katika nchi yote ya nchini India.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni