JWTZ YAPANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO IKIWEMO GOFU NCHINI .


sem1
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali  Venance mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa Mashindano  ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo  Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
sem2
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali  Venance mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mrisho Sarakikya  wakati akishiriki Mashindano  ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
sem3
Mshindi wa kundi la Wanawake wa Mashindano  ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo  Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
sem5
Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano  ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo  Angel Eaton  akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
sem6
Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano  ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo  ambaye pia alikuwa mwenyekiti  wa kamati ya Maandalizi Dkt Edmund Mndolwa   akiwa katika harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
sem7
Baadhi ya Wasanii wa Ngoma kutoka kundi la Ngoma la Jeshi la  Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Band Coy wakitumbuiza  wakati  wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo   Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
…………………………………………………………………
Na Luteni Selemani  Semunyu  JWTZ
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania  kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya kanda  katika maeneo mbalimbali nchini kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati akifunga  Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo  Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.
Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa  Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa kujenga Viwanja vya kanda  na Lugalo kuwa na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la Michezo kwa Wananchi.
Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo  alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya Gofu lakini bado  wataendeleza Uwanja wa Lugalo  pale ambapo  watangulizi wake wameishia  na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.
“ Nilikuwa naongea na mwenyekiti kamati ya mashindano Dk  Edmund Mndolwa alinidokeza tatizo la kukauka kwa Uwanja kipindi cha Kiangazi na kutochezeka Vizuri nimelichukua na tutalifanyia kazi  tunashukuru Afande waitara kwa Ubunifu na namshukuru Mtangulizi wangu Jenerali Mwamunyange kwa kuilea klabu kwa Mafanikio  nami kwa kushirikiana na Wanachama nitaendeleza ili klabu izidi kuimarika”. Alisema Jenerali Mabeyo.
Pia aliwashukuru Waandishio wa habari na wadau Mbali mbali katika kuitangaza na kufanikisha  shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa  na imejidhihirisha kutokana na Umati mkubwa uliojitokeza katika maadhimisho hayo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali  Mstaafu Michael Luwongo alisema  katika kipindi cha Miaka 10 wamepata mafanikio makubwa hivyo sasa licha ya kufanya uwanja kuwa na hadhi ya kimataifa na mpango maalumu wa ukuzaji vipaji kwa watoton lakini walenga kupata viwanja kwa ajili ya Michezo mingine ikiwemo kuogelea.
Aliongeza kuwa Lugalo itabaki kitovu cha  Ukuzaji vipaji kutokana mpango maalum wa watoto ambao idadi yao sasa inafikia zaidi ya 50 ambayo ni kubwa ukilinganisha na Klabu zote nchini.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo Dkt Edmund Mndolwa alisema wanashukuru JWTZ   kwa kutoa  fursa kwa raia kushiriki katika Klabu hiyo hali iliyoondoa adha kubwa kwa wazalendo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni