Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph. Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.
Kutokana na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.
Katika siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.
Semina hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni