LEMA ARUDISHWA RUMANDE MPAKA FEBRUARY 10

Kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na mkewe Neema Lema leo Ijumaa February 3 imesikilizwa tena kwenye mahakama kuu ya Arusha ambapo

Pingamizi lililowekwa na wakili wa Mbunge Lema  kuhusu hati ya shtaka la upande wa jamhuri kuwa batili katika kesi inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema na mke wake Neema Lema  limewasilishwa

Pingamizi limeeleza Lema na mke wake walituma ujumbe unaosema :Tutakudhibiti kama arabuni wanavyodhibiti mashoga"wakati hati ya mashtaka  imenakiliwa ujumbe ambao mtuhumiwa ameutumia bali ujumbe mtuhumiwa alioutuma unapaswa kupewa jina 

Wakili John Malya amesema moja ya kosa ni  kwenye hati ya mashtaka iliyotolewa na wakili wa serikali  wakati wakutaja wadhifa wa viongozi katika upande wa mbunge wameandika mbunge badala yakuandika mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema

Malya Amesema sheria haipaswi kubagua kwani mshtaki ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametajwa cheo chake na Lema ametajwa bila cheo chake

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo John Baro amehairisha kesi hiyo hadi February 10 mwaka huu ambapo atatolewa uamuzi pingamizi hilo.Lema amerudishwa rumande

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni