ANGELINA JOLIE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSIANA NA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKE


Muigizaji Angelina Jolie amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na wakati mgumu wa kuvunjika ndoa yake na Brad Pitt pamoja na madhara yaliyowapata watoto wao sita.

Nyota huyo wa Hollywood yupo nchini Cambodia akiwa na watoto wake kupromoti filamu yake mpya, alionekana kupatwa na majozi alipoulizwa kuhusiana kuvunjika kwa ndoa yake.

Jolie alisema hataki kusema zaidi kuhusiana na jambo hilo, na kueleza kuwa ilikuwa ni wakati mgumu lakini wao bado ni familia na wataendelea daima kuwa familia.
                           Angelina Jolie akiwa na watoto wake sita katika nchi ya Cambodia

Angelina Jolie akiwa na watoto wake sita wakiongea na mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni