Serikali
 kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  Dar es Salaam (DAWASA) 
inatekeleza mradi wenye thamani ya bilioni 18 unaolenga kuondoa 
changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Kauli
 hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa ufundi na uendeshaji wa Mamlaka 
hiyo Bw. Romanus Mwangingo wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika
 eneo la Kimbiji ambako ndipo mradi huo unapotekelezwa .
“Mkandarasi
 anaendelea na kazi  na ameleta mabomba yote na amechimba visima 15 na 
vitazalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na mradi 
unatarajiwa kukamilika machi 2017” Alisisistiza Mwangingo.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 85 na 
utakapokamilika maeneo ya Kigamboni,Temeke,Ilala na Jiji la Dar es 
salaam kwa ujumla yatanufaika kwa kupata huduma ya maji.
Kwa
 upande wa miradi  mingine kama ule wa ujenzi wa Bomba kutoka Ruvu juu 
hadi kimara Mwangingo amesema  ulikamilika mwezi oktoba 2016 na 
uzalishaji wa majaribio unaendelea.
Mradi
 huo wenye thamani ya dola za marekani  milioni 59 ni moja ya mikakati 
ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam 
wanapata huduma ya maji safi na salama. na kuondokana na changamoto 
hiyo. .
Aidha mradi huo utawezesha kiwango cha maji kufikia lita milioni 196 kwa
 siku kutoka lita milioni 82 za awali.
Kwa
 upande wake Bw.Salum  Hamis mkazi wa mbagala amepongeza miradi ya maji 
inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kwa kuwa imekuwa
 chachu ya maendeleo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa miradi hiyo imechochea  kupunguza tatizo la maji   na 
imewawezesha wananchi kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi na
 hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
Katika
 kukabilina na tatizo la miundombinu ya maji taka katika Jiji la Dar es 
salaam mamlaka hiyo iko katika mchakato wa kuanza ujenzi wa mtambo 
mkubwa wa kuchuja maji taka katika  eneo la Jangwani  na kuboresha mfumo
 wa maji taka katikati ya Jiji.
Mradi
 mwingine ni ule wa upanuzi wa ruvu chini ambao umekamilika kwa asilimia
 mia moja na utawezesha upatikanaji wa maji kufikia lita milioni 270 kwa
 siku kutoka milioni 180 kabla ya mradi huo haujatekelezwa.
Majukumu
 ya DAWASA  ni kumiliki miundombinu ya maji safi na maji taka kwa niaba 
ya Serikali, kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka Dar es
 salaam, kugharimia,kupanga mipango na kusimamia upanuzi wa huduma na 
kuishauri Serikali kuhusu masuala ya huduma ya maji safi na maji taka 
Jijini  Dar es salaam.
Mkurugenzi
 wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es
 Salaam (DAWASA), Mhandisi Romanus Mwang'ingo  akiwaeleza waandishi wa 
habari kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa changamoto ya 
upatikanaji wa maji katika  Jiji la Dar es salaam  inapatiwa ufumbuzi wa
 kudumu mara baada  ya kukamilika kwa miradi ya Ruvu Juu na Chini pamoja
 na ule wa uchimbaji wa Visima Virefu katika eneo la Kimbiji  
vitakavyozalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na 
Viunga vyake likiwemo eneo la Kigamboni.
Msimamizi
 wa mradi huo toka  Kampuni ya Serengeti Ltd Bw.MehrdadTalik (katikati) 
akisitiza Jambo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji 
Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Romanus 
03.Mwang'ingo  (kushoto) wakati wa ziara ya waandishi wa habari 
kutembelea mradi wa uchimbaji Visima virefu katika eneo la Kimbiji kulia
 ni mshauri wa mradi huo Bw. Roland Chombo.
Meneja
 Uhusiano wa DAWASA Bi Neli Msuya akieleza kwa waandishi wa habari faida
 za miradi inayoibuliwa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wananchi 
katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es 
salaam.
Maji
 yakitoka kwenye moja ya Kisima Kirefu kilichochimbwa katika eneo la 
Kimbiji unakotekelezwa mradi mkubwa wa unaolenga kutatua changamoto ya 
maji katika Jiji la Dar es salaam.
Mtambo unaotumika kuchoronga Visima Virefu ukiwa katika eneo la Kimbiji unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu.
Mwenyekiti
 wa Kamati ya Mladi,Salum Selenge akionesha tanki linalotumika kuhifadhi
 maji katika miradi iliyobuniwa na DAWASA katika eneo la mbagala na 
kuendeshwa na wananchi wenyewe ikiwa ni mkakati wa Mamlaka hiyo kuibua 
miradi ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar 
es salaam.
Sehemu ya Kisima kama inavyoonekana katika .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni