ZIARA YA MAJALIWA BABATI NA MBULU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mnada wa Haydom mkoani Manyara, Februari 20, 2017. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017. Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafa, Mama Sanka baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya wilaya ya Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni