TEA YASAINI MAKUBALIANO YA KUFADHILI MIRADI YA ELIMU NA SUNSHINE GROUP LTD.


1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA ), (kulia), Graceana Shirima akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Sunshine Group Ltd kutoka China wa miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili Miradi ya elimu nchini.

2
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun Ltd kutoka China akizungumza jambo kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Sunshine Group Ltd kutoka China wa miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili Miradi ya elimu nchini (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima.
3
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA ),Bi  Sylvia Lupembe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
4
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA  ), (kushoto), Graceana Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Kapuni ya Sunshine Group Ltd kutoka China (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Sunshine Group Ltd kutoka China wa miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili Miradi ya elimu nchini.
6
5
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
DSC_0014
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA ), (kushoto), Graceana Shirima akijibu maswali kwa waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo
7
Picha ya pamoja.
………………………………………………….
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha
elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.
“Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara
ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.
 Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Alisema kampuni yake imeingia Tanzania mwaka 2012 na tayari imetumia zaidi ya Dola 500,000 za Marekani katika elimu kwa miaka mitano ya uwepo wao hapa Tanzania.
“Tumedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha mazingira ya upatikanaji wa elimu yanakuwa rafiki na yenye kuvutia. Tunaamini TEA watatusaidia kuzifikia shule zenye uhitaji zaidi ili watoto wetu wapate elimu
bora kwa ajili ya kujenga taifa imara,” alisema Sun.
Miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni