Wakazi
 wa jiji la Mwanza wamezifurahia simu za kisasa za Smart Bomba ambazo 
zilizinduliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania hivi 
karibuni,Simu hizo zinazidi kuchangamkiwa na wananchi wengi hususani 
wakazi wa maeneo ya jiji la Mwanza na wanaozunguka mkoa huo ambapo 
wameshukuru kwa hatua hiyo ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta
 ya mawasiliano nchini.
Wakiongea
 kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo 
inayoendelea mkoani Mwanza,baadhi ya wananchi wamesema kuwa hatua ya 
kampuni hiyo kuingiza sokoni simu za kisasa za Smart Bomba 
zinazopatikana kwa gharama nafuu imedhihirisha dhamira ya kweli ya 
kampuni hiyo ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.
Bw.Focus
 Phabian mmoja wa wananchi ambaye amenunua simu hiyo akiongea kwa niaba 
ya wenzake alisema kuwa Smart Phone ni mkombozi wa mawasiliano ya kisasa
 kwa kuwa licha ya kuwa na unafuu wa bei pia imetengenezwa kwa kuendana 
sambamba na mazingira halisi ya watanzania.
“Simu
 ya Smart Bomba licha ya kuuzwa kwa shilingi 99,000 ambazo ni nafuu kwa 
watanzania wengi programu zake zinapatikana katika lugha ya taifa ya 
Kiswahili bila kusahau muundo wake unaowezesha kupata interneti yenye 
kasi kubwa ya Vodacom na kupiga picha zenye ubora wa hali ya juu 
.”Alisema.
“Watanzania
 wengi hivi sasa wana kiu ya kupata taarifa mbalimbali zinazotokea papo 
kwa papo na kujiunga pia na progamu za simu zinazorahisisha mawasliano 
kama whasap hivyo kwa Smart Bomba wengi watamudu kutumia simu za kisasa 
za intanenti ambazo zinauzwa kwa bei nafuu na zilizotengenezwa kwa 
kulenga mazingira halisi ya kitanzania”,Alisema Phabian.
Mkuu
 wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya ziwa,Ayoub 
Kalufya,alisema kuwa tangu simu hizi ziingizwe sokoni wiki moja 
iliyopita kumekuwepo na mwitikio mzuri wa wananchi ambao wamekuwa 
wakizinunua ili kuingia katika ulimwengu wa kidigitali.
“Smart
 Phone mbali na kuwa na unafuu wa bei pia inaambatana na ofa ya mteja 
anayenunua simu kuunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za 
bure kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo
 kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti i yenye 
kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote”,Alisema Kalufya.
Kalufya
 aliongeza “wakati ni huu kwa wakazi wa jiji la Mwanza mikoa mingine ya 
kanda ya ziwa makundi kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya 
Smart Bomba kwa gharama nafuu na kufurahia mawasiliano ya kisasa”.
Mkuu
 wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa ,Ayubu Kalufya akiitambulisha simu ya
 Smart Bomba kwa wakazi wa jijini Mwanza jana, kulia ni Mkuu wa Maduka 
ya Rejareja wa kampuni hiyo,Brigite Steven. 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiiangalia simu aina ya Smart Bomba, wakati wa utambulisho wa simu hiyo jijini humo.
Baahi
 ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Ziwa wakiandamana kwenye 
barabara ya Kenyatta jiji Mwanza jana, wakati wa kuitambulisha wa simu 
aina ya Smart Bomba kwa wakazi wa jiji hilo jana. 
Mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza Michael Alfred, akipokea simu
aina
 ya Smart Bomba ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania 
Kanda ya ziwa ,Ayubu Kalufya,baada ya kununua moja ya simu hizo wakati 
wa kuzitambulisha simu hizo jijini Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni