Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Charles Mwijage
amewataka watanzania kuwekeza katika mfumo unaoweza kutoa ajira za moja
kwa moja kwa vijana kama ilivyo katika kampuni ya Manjano Foundation.
Mwijage
amesema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
mafunzo ya wanafunzi 30 juu ya masuala ya urembo yanayoendeshwa ta
tasisi ya Manjano Foundation ya hapa hapa nchini.
“huyu
ni moja ya wawekezaji ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani
ameamua kuwekeza kwa kutengeneza bidhaa ambazo zinatumia malighafi
kutoka hapa hapa nchini na kuamua kuwawezesha wanawake wadogo kupata
mafunzo hili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema Waziri
Mwijage.
Mwijage
ameongeza kuwa mbali na Manjano foundation kutoa elimu ya ujasiliamali
kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe wa kujenga kiwanda mjini
kibaha ambapo tayari wameshapata ekeri tatu kwa ajili yakujenga Godown
ambalo litasaidia kufanya uzalishaji.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa
wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka tasisi hiyo wanaweza kuingiza
kiasi cha Milioni mbili mpaka tatu kwa mwezi.
Aidha
ametaja kuwa program hiyo katika mwaka hu itaweza kuwafikia wanawake
katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akipokelewa na
Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha
Nasser mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo kwa
wanawake ikiwa ni awamu ya pili.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akipata maelezo
kutoka kwa Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions,
Shekha Nasser kuhusu darasa linalotumika katika ufundishaji wa
wasichana hao leo katika ofisi ya Shear Illusion iliyopo jengo la
Millenium Tower jijini Dar
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza na
wanafunzi wa Manjano Academic mara baada ya kufika na kujionea mafunzo
hayo leo katika ofisi ya Shear Illusion jijini Dar
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza
wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi
ijulikanayo kama "Manjano Dream Makers" kwa awamu ya pili iliyozinduliwa
leo na waziri huyo katika ukumbi wa LAPF Millenium Towers jijini Dar es
Salaam leo.
Mwasisi
wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser
akizungumza kuhusu uzinduzi rasmi wa program ya ajira kupitia tasnia
ndogo ya urembo pamoja na kufanya utambulisho kwa wageni waalikwa.
Afisa
Kutoka TFDA Bi. Grace Shimwela akizungumzia umuhimu wa kupata vibali
vya urembo "Cosmetics and Personal Care" kwa wanawake walioko na ambao
wamemaliza progamu mbalimbali za mafunzo kutoka kwa Manjano Dream Maker
ili kuwasaidia pale wanapoanza kujitegemea
Jokate Mwegelo akizungumza jambo kwenye ufunguzi huo
Mshiriki
mmoja aliyenufaika na Taasisi ya Manjano, Josephine Rwetela
akizungumzia umuhimu wa kutengeneza ajira kupitia Tasnia ndogo ya Urembo
nchini.
Mkurugenzi
wa GS1 Tanzania, Fatma Khange akitoa maneno ya shukrani kwa wageni
waalikwa pamoja na wanawake wanaoshiri kwenye mafunzo hayo
yaliyoziduliwa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.
Charles Mwijage.
Baadhi ya washiriki walioudhuria katika uzinduzi huo
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akimkabidhi
cheti Mkurugenzi Mtendaji 8020 Fashion na Mentor wa Taasisi ya Manjano
Foundation, Shamim Mwasha
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akimkabidhi cheni
Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation, Mboni Masimba
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akimkabidhi
cheti Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation, Mariam Marion Ndaba
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akiwa kwenye picha ya pamoja na Manjano Academic
Mgeni
rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akiwa kwenye picha ya pamoja na Dream Makers.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni