MZEE WA UPAKO ASEMA MVUA HAINYESHI JIJINI DAR ILI BARABARA IANYOENDA KANISANI KWAKE IKAMILIKE

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo ametoa mpya jana baada jana kusema kuwa kitendo cha mvua kuchelewa kunyesha jijini ni kusudio la Mungu ili kutoathiri ujenzi wa barabara inayokwenda kanisani kwake.
Lusekelo ambaye ni maarufu kama “Mzee wa Upako” alitoa kauli hiyo katika ibada iliyofanyika jana kwenye makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es salaam.
“Maisha ni Mungu. Hata kama una kazi na unafanya bidii, kama huna Mungu huwezi kufanikiwa. Hata kama watu wakikudhihaki, wakikusema na uongo, usilie. Sasa wewe ukikosa hela kidogo unapiga kelele utafikiri mjusi kabanwa na mlango. “Hapa juzi tu watu walikuwa wanalalamika kuwa mvua hakuna na wakaniuliza mbona siombei mvua. Nilichowajibu ni kuwa mimi mwenyewe nafurahia mvua isinyeshe hadi barabara ile itakapomalizika na haitanyesha mpaka itakapokwisha kutengenezwa,” alisema.
Ujenzi wa barabara hiyo kutoka Ubungo Kibangu hadi Riverside kwa kiwango cha lami ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais John Magufuli wakati alipomtembelea Mchungaji Lusekelo kanisani kwake, Juni 5 mwaka jana.
Agizo la ujenzi wa barabara hiyo ambalo Rais Magufuli alimpa Meneja wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam, limefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa, na hadi sasa karibu nusu ya barabara hiyo imeshakamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni