Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
amewataja majina mtandao wa wauza unga au dawa za kulevya wakiwemo
maofisa 9 wa jeshi la polisi mkoani kwake na wasanii wa mziki wa bongo
flava na movie.
Wapo pia ambao wako ndani wanashikiliwa na jeshi la polisi lakini
wasanii hao wote wameambiwa kureport kituo cha polisi bila shurti.
Nao hao maofisa tisa amempa siku 7
kamanda Siro kuwawajibisha na kama hata fanya hivyo basi kamanda Siro
awajibike mwenyewe katika hilo.
Na ameahaidi kuendelea na mapambano hayo ya kusaka mtandao wote katika
mkoa wake aidha pia amesema yupo tayari kuacha kazi ama kufa kwa ajili
ya hilo.
Ameyasema hayo muda huu katika ofisi yake akiwa na waandishi wa habari. # RFA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni