Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo anayeapishwa leo, jana aliwaaga waumini wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Segerea akisema amejifunza mengi kutoka kwao.
Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais John Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Davis Mwamunyange kustaafu.
Akizungumza baada ya ibada jana, Jenerali Mabeyo alisema katika kipindi cha miaka 12 alichoishi Segerea amejifunza mengi, ikiwamo namna ya kuishi na watu kwa amani.
“Nikiri kwamba nimejifunza mambo mengi kutoka kwenu waumini wenzangu na wakazi wote wa Segerea, mmekuwa msaada mkubwa kwangu,” alisema.
Alisema aliyojifunza yamesaidia kufanya ateuliwe na Rais kushika wadhifa huo mpya na kwamba, ataendelea kushirikiana na wakazi hao bila kujali umri, jinsi wala tofauti ya kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni