CRISTIANO RONALDO AMNUNULIA ZAWADI ZA VALENTINE MPENZI WAKE GEORGINA RODRIGUEZ

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez, amepata Siku ya Wapendanao bora baada ya kununuliwa vitu kadhaa Jijini Madrid.

Wawili hao walibainisha wazi mahusiano yao kwa mara ya kwanza Novemba huko Disneyland Paris, na tangu hapo imekuwa kawaida kuwaona pamoja mara kwa mara.

Nyota huyo wa Real Madrid, Ronaldo alipigwa picha jana Jijini Madrid akinunua vitu dukani na kuibuka na mifuko yenye zawadi za Valentine za mpenzi wake Rodriguez.
   Cristiano Ronaldo akiwa ameshika mfuko wenye zawadi alizomnunulia mpenzi wake Georgina
    Cristiano Ronaldo akifungua mlango wa gari lake baada ya kumaliza kufanya manunuzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni