Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Nianjema, Bagamoyo ,Ally Swalehe akizungumzia changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo uhaba wa madawati . (picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nianjema, Bagamoyo wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa msaada kutoka kwa mkurugenzi wa shule za Feza kwa kushirikiana na taasisi ya Time to Help. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nianjema, Bagamoyo wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa msaada kutoka kwa mkurugenzi wa shule za Feza kwa kushirikiana na taasisi ya Time to Help. (picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
SHULE ya msingi Nianjema,Bagamoyo, Pwani inakabiliwa na changamoto ya mlundikano wa wanafunzi wa darasa la awali ambapo kwasasa wapo 360 katika darasa hilo.
Aidha katika darasa la kwanza hadi la sita wanasoma wanafunzi zaidi ya 100 kila darasa hali inayosababisha kusoma kwa awamu mbili kwa siku na wengine kukaa chini.
Akizungumzia changamoto hiyo, kaimu mwalimu mkuu shuleni hapo, Ally Swalehe, alisema tatizo hilo limesababishwa na ongezeko la uandikishaji kwa darasa la awali na la kwanza.
Alieleza kwamba, kutokana na mfumo wa elimu bila malipo wazazi wamejitokeza kuandikisha watoto wao kwa wingi na kufikia asilimia 32.
“Mlundikano umezidi kutokana na ongezeko la uandikishwaji tofauti na miaka ya nyuma “alisema.
Mwalimu Swalehe alisema, wamechukua hatua ya kuwagawa wanafunzi wa awali kwenye awamu mbili ambapo wanasoma 180 katika awamu mbili.
Katika darasa la kwanza wanaingia asubuhi darasa la pili jioni, darasa la 4 asubuhi la 3 jioni, huku la sita likiingia asubuhi na la tano jioni.
Kwa mujibu wa mwalimu Swalehe,kiutararibu na muongozo wa sekta ya elimu kila darasa linatakiwa kuwa na wanafunzi 45 badala ya 100-360 .
Hata hivyo alielezea, kwasasa kuna madawati 436, yanahitajika 723 na upungufu ni 287 ,ambapo vyumba vya madarasa vipo 12 upungufu 28 mahitaji 40.
Nae mbunge wa jimbo la Bagamoyo, dk. Shukuru Kawambwa, alisema jukumu la kutatua changamoto za sekta ya elimu ni la jamii,wadau pasipo kuiachia serikali pekee.
Dk. Kawambwa alisema anaendelea kuzungumza na wadau mbalimbali ili kushirikiana nao kuondoa changamoto zilizopo s/m Nianjema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni