Muigizaji filamu nyota Mmarekani,
Harrison Ford, 74, amenusurika kupata ajali ya ndege aliyokuwa
akiiendesha huko California, nchini Marekani.
Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea
pale alipopewa maelekezo ya kutua katika njia ya kutulia ndege katika
uwanja wa ndege wa John Wayne uliopo kaunti ya Orange.
Hata hivyo Ford alitua vibaya katika
njia ya ndege zilizopakiwa na kupitiliza karibu na ndege ya American Airlines iliyokuwa na
abiria 110 na watumishi.
Muigizaji filamu Harrison Ford akiangalia ndege yake baada ya kutua asipostahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni