Mkuu wa Mawasiliano Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Innocent Mungy akizungumza katika bonanza hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
…………………………………………………………………….
Na Hassan Silayo
Zaidi ya wananchi 500 wakiwemo waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano Serikalini wamepima afya katika bonanza lililoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano serikalini, jukwaa la wahariri na klabu ya waandishi Dar es Salaam.
Bonanza hilo lililohusisha pia uchangiaji damu kwa hiari na ufanyaji mazoezi ya viungo ili kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Akiongea mara baada ya kupima afya Sharifa Hussein mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam amesema kuwa anawapongeza waliofanya uratibu wa kupeleka madaktari kwani imewapa fursa ya kujua hali za afya yao pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
“Niliona tangazo kuhusu upimaji afya hapa, nimekuja nimepima nimepata majibu pamoja na ushauri, kwakweli nawashukuru waandaaji wa shughuli hii, imesaidia wengi kujua hali za afya zao na sasa ni jukumu letu kwenda kufanyia kazi yale tuliyoambiwa baada ya mati Watoto Alisema Bi.Sharifa.
Akiongea baada ya kumaliza programu ya mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa watanzania hawana budi kufanya mazoezi mara kwa mara kwani inasaidia kupunguza gharama zinazoweza kutumika kutibu magonjwa yanayoweza kusababishwa na kutofanya mazoezi ambayo yamekuwa yakisumbua wengi hasa gharama za matibabu yake.
Naye Mwenyekiti wa Chama chaMaafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy amesema kuwa wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuunga mkono agizo la makamu wa rais makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambuka.
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF) Teophil Makunga aliwasisitiza wanannchi kuweka programu binafsi za kufanya mazoezi kwani mazoezi yana saidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mara kwa mara pia yanasadia kufikiri na kufanya mambo vizuri.
Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukizwa Dkt Digna Siriwa Alisema kuwa kutokana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema kuwa kwa mwaka 2008 asilimia 63 ya watu ulimwenguni walikufa kwa mgonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Presha, Sukari, Kansa pamoja na magonjwa ya mfuko wa hewa ambayo yanaweza kuzuiwa kwa kufanya mazoezi
Bonanza hilo limeandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini, Jukwaa la Wahariri, Klabu ya Waandishi wa habari wa Dar es salaam pamoja na kuratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni