Vodacom yazindua simu mpya ya Smart Bomba
· Matumizi yake yapo kwenye lugha ya Kiswahili
· Inauzwa ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 30 za buree kwa miezi 3!
Dar
es Salaam,Jumatano Februari 03,2017:Sasa ni wakati wa watanzania
kufurahia ubunifu wa kiteknolojia wa mawasiliano unaoendana sambamba na
mazingira yao halisi na kufurahia kupata taarifa na burudani kwa njia ya
interneti ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,mtandao unaoongoza
nchini wataweza kujipatia simu za kisasa zinazotumia interneti aina ya
Smart Bomba.
Simu
za Smart Bomba ambazo zimezinduliwa rasmi nchini leo zinapatikana kwa
gharama nafuu ya shilingi 99,000/-muundo wa matumizi yake uko katika
lugha ya taifa ya Kiswahili pia zinanunuliwa zikiwa tayari
zimeunganishwa na kifurushi cha interneti chenye GB 10 za buree kwa
mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa
ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi
kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote.
Mbali
na muundo wa matumizi ya simu hii kuwa katika lugha ya Kiswahili na
kwendana na mazingira halisi ya maisha ya watanzania walio wengi,simu
za Smart Bomba zina umbo la kuvutia,nyepesi na zina kioo cha mbele,cha
ukubwa wa kutosha,zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya android
inaongeza kasi ya kuperuzi internet,inayo kamera ya kurekodi na kupiga
picha kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu vilevile inao mfumo wa
utambuzi wa ramani ya maeneo mbalimbali ujulikanao kama GPS ambao unatoa
maelekezo kuonyesha mahali mtu alipo na mahali aendapo kwa urahisi
hususani madereva wa teksi ambao huwapeleka wateja wao sehemu mbalimbali
wasiozijua,na zimeunganishwa na program za simu za kurahisisha Maisha
za Vodacom kama vile M-Paper.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa simu hii,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania
kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama,alisema wakati ni huu wa kila
mtanzania kuweza kufurahia matumizi ya simu za kisasa zinazotumia
internet (Smart Phones) kwa ajili ya kupata taarifa na burudani kutoka
mitandaoni kutokana na kupatikana kwa mara ya kwanza kwa gharama nafuu
nchini.
“Kuingia
sokoni kwa simu za Smart Bomba za gharama nafuu na zilizotengenezwa
kwendana sambamba na mazingira na Maisha ya watanzania walio wengi
zikiwa zimeunganishwa na GB 30 kwa matumizi ya miezi 3 ya mwanzoni ni
ofa ya kipekee ambayo imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio
wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua”.
Mkama
aliongeza kusema “Hivi sasa tuko katika zama za kidigitali ambayo
mawasiliano ya watu wengi yanafanyika kupitia mitandao ya kijamii ,hivyo
wananchi wengi wakiwa na simu za kisasa zinazotumia internet wanaweza
kufanya mambo mengi kwa urahisi na haraka kuanzua kwenye biashara,kupata
taarifa mbalimbali,kutumiana salamu na kupata burudani za muziki na
sinema kutoka mitandaoni”.Alisema.
Alisema
wakati ni huu kwa makundi mbalimbali ya watanzania katika jamii
kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya Smart Bomba kwa gharama
nafuu na kuwa mtu wa kisasa anayeenda na wakati na simu hizi zinatukuwa
zinapatikana kwenye maduka yote yanayouza simu nchini na zina waranti
ya mwaka mmoja.
Kwa
kutambua kuwa kundi kubwa kwenye jamii linahitaji matumizi ya intanenti
kupata burudani na kupakua muziki hususani muziki wa Bongo
Flava,uzinduzi wa simu hii na matangazo yake yamemuhusisha mwanamuzi
nguli wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo,Diamond Platnumz aliwapongeza Vodacom kwa
kuingiza sokoni simu ya kisasa ya Smart Bomba ambayo imelenga kutumiwa
na wananchi wengi kwa kuwa ina unafuu na inaendana na Maisha halisi ya
watanzania. “Sasa ni wakati wa kila mtanzania kwenda kidigitali kwa ku
chart,kupata nyimbo za wazipendazo live kupitia simu zao na kupakua
filamu wazipendazo ,kutumiana salamu na picha kwa njia ya simu,kuperuzi
internet na kupata taarifa na burudani kupitia ncha za vidole vyao na
haya yote yanapatikana katika mtandao mkubwa nchini wa Vodacom pekee.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama(kushoto) akimshuhudia Balozi
wa kampuni hiyo,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond
Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo na
waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina
ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa
shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya
GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.
Balozi
wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul”
Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam
leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart
Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi
99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za
buree kwa kipindi cha miezi 3. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama.
Balozi
wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul”
Diamond Platinumz” akiwaburudisha wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es
Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye
matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu
iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa
kipindi cha miezi 3.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni