Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez
akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Maruwa wilaya ya Moshi vijijini
mara baada ya kuwasili kwa ajili ya shughuli ya kuotesha miti 120 katika
eneo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na
wageni wengine wakitizama mnara wa kumbukumbu uliowekwa katika eneo hilo
baada ya kufanyika kwa shughuli za uoteshaji miti 1510 mwaka 2015.
Kaimu
Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la kuhifadhi Mazingira
(TEACA) Adoncome Mcharo akitoa taarifa fupi ya ukuaji wa miti
iliyooteshwa katika eneo na nusu maili ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro kwa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na
ujumbe wake (hawapo pichani)
Kaimu
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya TAifa ya Mlima Kilimajaro (KINAPA) Charles
Ngendo akizungumza kabla ya kuanza zoezi la uoteshaji miti katika eneo
hilo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi Celestine
Mushi akionesha eneo ambalo lilipandwa miti na tayari imeanza kukua.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa na
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini
Hoyce Temu wakitizama eneo lililooteshwa miti katika Hifadhi ya Taifa ya
Mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi
Celestine Mushi akitoa maelekezo eneo jingine lilaotakiwa kuoteshwa miti katika Hifadhi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi
Celestine Mushi akiwa amebeba iche ya miti kwa ajili ya kutoesha katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi
Celestine Mushi akiotesha miche ya miti katika eneo hilo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez
akiotesha miti katika eneo hilo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akimwagia maji miti aliyootesha katika eneo hilo.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngendo akiotesha mti katika eneo hilo.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Kimataifa (UN) nchini ,Hoyce Temu
akiotesha mti na kumwagia maji wakati wa zoezi la kuotesha miti katika
eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiotesha mti katika eneo hilo huku balozi Mushi akishuhudia.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez kwa
pamoja na Balozi Mushi wakimwagia maji katika mti uliooteshwa katika
eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni