Na Mahmoud Ahmad,Monduli
Ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho
Gambo katika vijiji vya
Mbaashi na Selela amekumbana na mgogoro wa matumizi ya
ardhi katika
kijiji cha Selela ambapo wananchi wamemweleza kuwa halmashauri ya kijiji
hicho imetoa sehemu ya eneo la shule ambalo lilikua ni kiwanja cha
mpita na kulifanya kuwa soko ilhali kiwanja cha michezo kuhamishiwa
sehemu ingine.
Hayo
yaliibuka baada ya mkuu wa mkoa Mh Gambo kupokea maswali na
kero za wananchi ambapo wananchi wengi walionyesha kutoridhishwa na
maamuzi mengi yaliyofanywa na halmashauri ya kijiji hicho juu ya
matumizi yenye manufaa ya ardhi.
Mh. Gambo
ameitaka halmashauri ya kijiji hicho kurudisha eneo la
michezo eneo la shule na soko lipelekwe mbali na maeneo hayo ya shule
ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi.
Pia
amemtaka afisa elimu msingi Bi
Theresia Kyara na mdhibiti ubora wa shule kufika shuleni hapo na kijiji
cha Nadosoito ili kuwaelekeza wanakijiji juu ya ubora wa shule
zinazotakiwa na serikali kwani halmashauri ya kijiji cha Nadosoito kipo
katika hatua za awali za ujenzi wa shule ya msingi.
Mh Gambo
alipokea lalamiko la Mlemavu Aloyce Mollel kuwa kwa
miaka Zaidi ya saba amekua anaomba halmashauri ya kijiji cha Selela
impatie eneo la kuishi na mpaka sasa ameshaandika barua zaidi ya kumi na
saba bila majibu
Katika
hali isiyo ya kawaida Mh Gambo alimwita
mwenyekiti wa kijiji na Afisa Ardhi wa halmashauri ya Monduli Bw. Adili
Mwanga ambapo kwa pamoja waliamua ndani ya wiki tatu watakua wamemaliza
kupima ardhi ya kijiji hicho na watakua tayari kwa kuviuza kwa
wananchi, Mh Gambo aliamua kumlipia kabisa mlemavu huyo kiasi cha
shilingi Laki moja na nusu ikiwa ni gharama ya kiwanja kimoja kama
makisio ya gharama yalivyotolewa na mtaalamu huyo wa ardhi.
Naye
mbunge wa Monduli Mh Julius Kallanga Laizer amemshukuru sana
mkuu huyo wa mkoa kwa namna anavyopambana kutatua kero za wananchi wa
Arusha na anaishukuru sana serikali ya Mh Dr John Pombe Magufuli kwani
utekelezaji wa ilani ya CCM unaonekana kutoa majawabu kwa matatizo mengi
ya wananchi.
Wilaya ya
Monduli ina jumla ya migogoro ya ardhi mikubwa mitano
(5). Migogoro mitatu inahusu mipaka ya wilaya ya Arumeru na
Monduli,wilaya ya Babati na Monduli na wilaya ya Longido na Monduli.
Migogoro hii ipo katika hatua nzuri ya utatuzi kwa kushirikiana na Ofisi
ya katibu tawala Mkoa wa Arusha.
Toka
awamu ya tano imeingia madarakani kumekua na mchakato wa
kufuta mashamba pori ambayo kwa muda mrefu yamekua hayaendelezwi. Ikiwa
hadi sasa mashamba 31 yameshafutiwa umiliki 13 na Rais wa Jamhuri ya
Muungano na 18 kwa ngazi ya kijiji.
Mkuu
wa mkoa akifungua nyumba ya mwalimu shule ya msingi
Mbaash
Wanafunzi shule ya msingi Selela wakimkaribisha mkuu wa
mkoa shuleni kwao
Mh
Gambo akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya waalimu na madara
mawili
Mh
Gambo akipokea zawadi toka kwa wananchi wa Selela
Kutoka
Kushoto ni mbunge wa Monduli Mh Julius Kallanga, Mh Mrisho Gambo na
mwisho ni Diwani kata ya Selela bwana Cuthbert Meena wakijadili
jambo
Baadhi
ya wananchi kata ya Selela wakimsikiliza Mh Gambo katika mkutano wa
hadhara
Bi
Namnyaki Lekule akitoa kero yake kwenye mkutano
Bwana
Aloyce Mollel akipokea fedha taslimu shilingi laki moja nusu ikiwa ni
mchango wa kumnunulia kijana huyo kiwanja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni