MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MJINI DUBAI




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na wajumbe wengine wa Jopo hilo mjini Dubai.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Siriel Shaidi Mchembe kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mrithi wa Mtawala wa Dubai Sheikh Hamdan Bin Mohamed bin Rashid Al Maktoum pamoja na wajumbe wa Jopo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jopo la Umoja wa Mtaifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi ulioanza tarehe 6 februari mjini Dubai.

................................................................

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria mkutano wa Jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi kama mmoja wa wajumbe wa jopo hilo.

Mkutano huu umefanyika mjini Dubai, Falme za Kiarabu na Ufunguzi rasmi ulihudhuriwa na Mrithi wa Mtawala wa Dubai Mtukufu Sheikh Hamdan Bin Mohammed Bin Rashid Al Maktoum pamoja na viongozi na wakuu wa Serikali wa Falme za Kiarabu .

Lengo la Mkutano huu ilikuwa ni kupitia Ripoti ya Kwanza ya Jopo hilo iliyowasilishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mwezi Septemba 2016. Mkutano huu wa Dubai, unategemea kutoa Ripoti ya Pili ambayo itatoa muelekeo wa namna Serikali zitashirikiana na wadau mbalimbali kama vile sekta binafsi, Asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo katika jitahada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.

Wajumbe wa Jopo hili, walipata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazomkabili mwanamke; pamoja na kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo yatakayoleta matokeo chanya katika kumuinua mwanamke kiuchumi. Mbali na kupendekeza maboresho ya Ripoti hiyo, wajumbe walijadili na kupendekeza hatua ambazo wadau watatakiwa kuchukua ili kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Tanzania kama nchi mwanachama ilipata fursa ya kutoa uzoefu wake jinsi Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wanawake hususani wale walio katika sekta isiyo rasmi; hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo wadogo wanawake ili kuhakikisha wanafaidika na mifumo ya kifedha na kijiditali kama vile kupata mikopo ya gharama nafuu; kuingizwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na huduma zingine.

Makamu wa Rais alisema pamoja na kila bara kuwa na changamoto zake, bado kuna umuhimu wa dunia kuhakikisha inaweka misingi madhubuti ya kuinua wanawake kiuchumi hasa kwa wanawake wa ngazi za chini ambao wengi wao wanaishii vijijini.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na mifumo ya sheria na sera zilizopo kuwa bado zinawanyima wanawake haki ya kurithi na kumiliki ardhi hata kama haki hizo zimewekwa kisheria."Hii inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, inayosababishwa na kuwepo kwa mianya kwenye hizo sheria na utendaji wa kubagua ambapo unaondoa ule mfumo rasmi wa kisheria unaotegemewa," alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema ushiriki mdogo wa wanawake ambao wengi ni wajasiriamali, katika kutumia mifumo ya kifedha ikiwemo mifumo mipya ya teknolojia ya fedha mtandao inachangia kuwafanya wanawake wakose mapato na hivyo kushindwa kufanikisha azma ya kuwezesha wanawake kiuchumi. Aliwaasa wanawake waungane na kuinuana wenyewe kwa wenyewe ili kuweza kutoachwa nyuma kwenye kufikia malengo yao ya kiuchumi na kwamba sambamba na utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya mwaka 2030.

Jopo hilo linatakiwa kuwasilisha ripoti yake ya Pili kwenye Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani mwezi Machi mwaka huu.

Mkutano huo ulileta washiriki takriban 45 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serikali, Taasisi binafsi, wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kumwezesha mwanamke kiuchumi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni