MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM MWITA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KUPITISHA BAJETI YA MWAKA 2016/17 AMBAYO NI SH.BILIONI 13.18



Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza na wajumbe wa baraza la madiwani wa jiji hilo katika Ukumbi wa Karimjee leo,wakati wa kupitisha makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji hilo,Sipora Liana na Naibu Meya wa Jiji,Mussa Kafana.(PICHA ZOTE NA Mahmoud Ahmad)



 Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana,akitoa taarifa ya makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. Kushoto kwake ni Meya wa Jiji hilo,Isaya Mwita na Naibu Meya,Mussa Kafana.

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji hilo.



 Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea (katikati) akiichambua bajeti ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakati walipokuwa wakiijadili katika baraza la madiwani wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo.Kulia ni Diwani wa Kata ya Mchafukoge,Mariam Ruliga na Diwani wa Kata ya Mbezi Luis,Humphrey Sambo


 Diwani wa Kata ya Tabata,Patrick Assenga (Chadema) akichangia katika kikao cha bajeti hiyo.
 Mbunge wa Temeke,Abdallah Mtolea,akichangia mada wakati wa kiako hicho cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.



 Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea (katikati) akichangia mada wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa jiji la Dar es Salaam kilichopitisha makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. katika ukumbi wa Karimjee leo. Kulia ni Mbunge wa Kigamboni,Dk.Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mbezi Luis,Humphrey Sambo na Mbunge wa Temeke,Abdallah Mtolea.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea (katikati) akichangia mada wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa jiji la Dar es Salaam kilichopitisha makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. katika ukumbi wa Karimjee leo. Kulia ni Mbunge wa Kigamboni,Dk.Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mbezi Luis,Humphrey Sambo na Mbunge wa Temeke,Abdallah Mtolea.

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea (Chadema),akifuarhia jambo na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Dk.Faustine Ndugulile (CCM) wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa Jiji la Dar es Salaam kujadili na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/17 ya jiji hilo katika Ukumbi wa Karimjee leo.


 Wakifurahia jambo katika kikao hicho wakati kikiendelea.

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akitoka chumba cha mikutano kwenye ukumbi wa Karimjee leo.



Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana, akitoka chumba cha mikutano baada ya kutoka kwenye kikao cha makisio ya bajeti ya jiji hilo kwenye ukumbi wa Karimjee leo.

NA ELISA SHUNDA,DAR
Baraza la Madiwani Jiji la Dar es salaam limepitisha kwa kauli moja makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya baraza hilo,Mkurugenzi wa Jiji,Sipora Liana alisema kuwa fedha hizo zinatokana na mapato ya vyanzo vya ndani  ambapo ni makisio ya bajeti kuanzia mwaka 2015/2016 ya utendaji kazi wa halmashauri ya jiji kwa miaka hiyo na mpango kazi kwa bajeti ya mwaka 2016/2017.
Aidha Liana amefafanua kuwa jumla ya makadirio ya mwaka wa fedha 2015/16 ni Sh.Milioni 13.177 ambapo Sh.Milioni 5.403 ni ruzuku kutoka serikali kuu huku Sh.Milioni 7.167 ni fedha zinatokana na vyanzo vya mapato ya ndani na salio anzia ni Sh.Milioni 332.135,katika kipindi cha Julai 2015 mpaka Juni 2016 kiasi cha Sh.Milioni 9.508 kilikusanywa ambacho ni sawa na asilimia 72.16 ya jumla ya bajeti.


''jumla ya Sh.Milioni 668.403 zitatumika kuwalipa watumishi wa jiji la Dar es salaam huku Sh.Milioni 4.518  fedha za miradi ya maendeleo ambapo jumla ya fedha 2.312 zilizotolewa na serikali kuu zinatarajiwa kuwalipa watumishi wa serikali ''Alisema Liana.

Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016/17 makisio ya bajeti katika jiji hilo yalikuwa ni Sh.Milioni 11.352 ambapo kati ya Sh. 3,595 ni ruzuku kutoka serikali na jumla ya Sh. 7.756 ambazo zimetokana na makusanyo ya kodi mbalimbali kama mapato ya ndani sawa na asilimia 60.53 ya bajeti yote .

Alisema kati ya Sh. Milioni 50 katika bajeti hiyo ziliweza kutumika katika kufanya tahimini na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya jiji hilo huku Sh. Milioni 20 zilitumika katika kuandaa mikakati ya jiji hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo .
 Naye Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,amewataka madiwani wa baraza hilo la Jiji kuwatumikia wananchi na kuziheshimu nafasi zao kwani kwa sasa wananchi wanataka maendeleo kwa kasi na kuangalia kero mbalimbali zinazolikabili jiji hilo na kuacha ushabiki wa kisiasa ambao utaleta mkwamo wa maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea alilitaka baraza hilo kutenga bajeti ya kuboresha huduma mbalimbali za jamii katika jiji hilo ikiwemo zahanati na kutaka madiwani wa kata hiyo kuwa na akidi ya wajumbe inayojitosheleza katika mikutano yake inapoamua kupitisha mambo ya msingi kama hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni