Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
Bwana na Bibi Alex wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi kampuni ya Star Times Tanzania
Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick 
Wafanyakazi wa Star Times Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  wakiwa wameshika maua
Meneja
 uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko 
wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni 
Valentine's na Star Times
KAMPUNI
 ya Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa
 zawadi kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".
Akizungumza
 na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa 
kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix 
Awino amesema Star Times inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi 
kupata chakula cha jioni na malazi ya Hotel ya kisasa.
“tunafurahi
 kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama 
sehemu ya upendo wetu kwao, kwa kuwapa promosheni na maudhui 
yanayoendana na wakati ,hivyo kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata 
malazi SeaScape,  Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika , Meya 
wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata 
kupumzika katika Hotel ya Morena”amesema Awino.
Kwa
 upande wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na 
Startimes, Nuezy Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja 
wa Star Times kupata nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama 
hiyo hili waweze kufurahi na wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi 
cha Star Times.
Amesema kuwa star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na kufurahia vipindi bomba vya kila siku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni