TAREHE 19.02.2017 MAJIRA YA SAA 7:25HRS ASUBUHI KATIKA STANDI YA KAMANGA FERI KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA STANSLAUS LUCAS, MIAKA 38 MKURYA NA MKAZI WA NYAKATO NATIONAL, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIFIKA HAPO KWENYE STANDI YA KAMANGA FERI MAJIRA TAJWA HAPO JUU AKIWA NA GARI LENYE NAMBA T.701 AINA YA NOAH, KISHA ALITOA BOKSI MOJA KUTOKA NDANI YA GARI LAKE NA KUWAKABIDHI MAWAKALA WA MAGARI YAENDAYO KIGOMA NA KUWAELEZA KUWA MZIGO WAKE ANAOMBA USHUSHWE KIBONDO. MAWAKALA WA MAGARI WALIPATA MASHAKA JUU YA HILO BOKSI NDIPO WALIMWOMBA MTUHUMIWA AWAELEZE KITU ALICHOKIWEKA NDANI YA BOKSI, LAKINI MTUHUMIWA HAKUWEZA KUELEZA KITU CHOCHOTE, NDIPO WALILIFUNGUA NA KULICHEKI NDANI NA KUONA LIKIWA LIMEJAA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI.
AIDHA BAADA BOKSI KUONEKANA LIKIWA LIMEWEKWA MIRUNGI, MAWAKALA WA MAAGARI WALIMSHIKILIA MTUHUMIWA KISHA WAKATOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMTIA NGUVUNI MTUHUMIWA PAMOJA NA KULIIFANYIA UPEKUZI GARI LAKE AMBAPO LILIKAMATWA BOKSI LINGINE LIKIWA NA MIRUNGI, AIDHA MABOKSI YOTE MAWILI YALIYOKAMATWA YALIKUWA NA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31.
KATIKA MAHOJIANO YA AWALI ALIYOFANYIWA MTUHUMIWA NA POLISI ALIKIRI KUWA NI KWELI AMEKUWA AKIJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA YA AINA YA MIRUNGI KWA MUDA MREFU, ALIDAI KUWA MIRUNGI AMEKUWA AKIITOLEA SIRARI NA KUISAMBAZA SEHEMU MBALIMBALI YA JIJI LA MWANZA NA MAENEO YA JIRANI, LAKINI ALIDAI KUWA MIRUNGI HIYO ALIYOKAMATWA NAYO ALIKUWA AKITAKA KUISAFIRISHA KWENDA KIBONDO MKOANI KIGOMA. POLISI WANAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA ILI KUWEZA KUBAINI MTANDAO WA WATU WENGINE ANAOSHIRIKIANA NAO KATIKA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWAPONGEZA MAWAKALA WA MAGARI WOTE WA STANDI YA KAMANGA FERI KWA USHIRIKIANO MZURI WA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA AMBAO WAMEUONESHA KWA WANANCHI, HIVYO ANAWASIHI WATU WOTE WA JIJI LA MWANZA WAIGE MFANO WA AINA KAMA HII. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI JUU YA WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA, UTUMIAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA HARAMU YA KULEVYA, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MANAMO TAREHE 18.02.2017 MAJIRA YA SAA 21:05HRS USIKU KATIKA MTAA WA IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKI KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATATU WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1. HAJI IDD MIAKA 34, MNYAMWEZI NA MKAZI WA IGOMBE AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 40, 2. VUMILIA CHARLES MIAKA 36, MSUKUMA NA MKAZI WA IGOMBE AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KIASI CHA LITA 10 NA 3.LEAH GILIGHA MIAKA 53, MSUKUMA NA MKAZI WA IGOMBE AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KIASI CHA LITA 06, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI POLISI WAKIWA KWENYE DORIA NA MIASKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU AMBAO WANAJIHUSISHA NA BIASHA HARAMU YA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA NA BHANGI. ASKARI WALIFANYA UPELELEZI KATIKA MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WATATU TAJWA HAPO JUU, AMBAPO WAWILI WALIKAMATWA WAKIWA NA POMBE AINA YA GONGO HUKU MMOJA AKIWA NA MISOKOTO YA BHANGI.
POLISI BADO WANAENDELEA NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATATU WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAO. AIDHA ASKARI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MISAKO KATIKA MAENEO HAYO ILI KUWEZA KUWAKAMATA WATU WENGINE AMBAO WANADAIWA KUWA WANAENDELEA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE AINA GONGO NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA MIRUNGI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA PAMOJA NA POMBE AINA YA GONGO KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI ANAWATAKA WANANCHI WAFANYE KAZI ZILIZO HALALI ILI WAWEZE KUJIEPUSHA NA MATATIZO, AIDHA ANAENDELEA KUWATAKA WANANCHI WOTE WA JIJI LA MWANZA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LAO ILI LIWEZE KUDHIBITI VYEMA UHALIFU KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni