FAO YATOA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 280 KATIKA MCHAKATO WA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998


1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi ( kushoto)  akizungumza kabla kutia saini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)  ya  kupitia upya   Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo  imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.       
2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi ( kushoto)  akiwa na  Mwakilishi wa Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero (kulia)  wakisaini hati ya makubaliano ya  kupitia upya   Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo  imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.        
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi ( kushoto)  akiwa na  Mwakilishi Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia)  wakibadilishana hati ya  makubaliano ya  kupitia upya  Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo  imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.
4
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akionesha kitabu cha  Sera ya Taifa ya Misitu ya Mwaka ya  1998 ambayo imepitwa na wakati kutokana na mabadailiko mengi kutokea nchini. Wengine ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi ( kushoto)  akiwa na  Mwakilishi Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia).
………………………………….
Serikali ya Tanzania na Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wameisaini  makubaliano ya kupitia upya  Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo  imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi amesema  mpango huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 280 ambazo zimetolewa na  FAO kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya Taifa  ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.
Amesema hatua hiyo imekuja   Kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998   inayotumika hadi hivi  sasa kupitwa na wakati yakiwemo  mabadiliko ya Kiuchumi, Kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi.
 Maj. Gen.  Gaudence ameeleza kuwa  kumekuwa na  ongezeko kubwa la  ufyekaji misitu na hivyo kumechangia  kupunguza uoto wa  asili kutoka hekta milioni 55.9 kwa  mwaka 1990 hadi kufikia hekta milioni  46 kwa sasa lakini Sera ya Misitu ni ile ile.
‘’ Sera ya Taifa ya Misitu ilishafanyiwa mapitio kuanzia mwaka 2009, Lakini kutokana na Sera hii kukaa kwa muda wa takribani Miaka 9 hadi hivi sasa tumegundua kuwa  baadhi ya wadau wengi hawakupata nafasi ya kutoa mawazo yao. Hata wale waliotoa mawazo yao mengi yameshapitwa na wakati.’’ Alisema Maj. Gen. Milanzi
Naye Mwakilishi Shirika  la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero amesema kuwa Mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na  kuwajengea uwezo watumishi kuweza  kukusanya taarifa nyingi ili  ziwezeshe kuboresha sera kupitia tafiti.
Aidha,Kafeero amesema kutokana na  mabadiliko hayo FAO itasaidia katika  kuhuisha sera  mpya ambayo itatoa majibu kwa changamoto zinazoikabili nchi hivi sasa na kukidhi mikataba ya kimaifa kama vile mabadiliko ya tabia ya nchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni