RAIS DONALD TRUMP AVISHAMBULIA TENA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Marekani Donald Trump amevishambulia tena vikali vyombo vya habari katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Florida.

Trump ameuambia umati uliohudhuria mkutano huo uliofanyika Melbourne kuwa vyombo vya habari havitaki kuripoti ukweli na vina agenda yao binafsi.

Aidha, Trump ametetea mafanikio yake akiwa kama rais hadi sasa kwa kusema, kuwa hali ya matumaini ya mafanikio imetamalaki katika maeneo yote ya Marekani.

Rais Trump pia alivishambulia vyombo vya habari katika mkutano wake na vyombo vya habari siku ya Alhamis, huku akikabiliwa na shinikizo la urais wake.
     Umati wa mashabiki wa rais Trump uliojitokeza kumsikiliza katika mkutano huo
      Rais Trump akimbusu mkewe Melania Trump wakati akimtambulisha katika mkutano huo
       Mke wa rais Trump, Melania Trump, akiongea katika mkutano huo baada ya kutambulishwa na mumewe 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni