WAKAZI WA KIRINYAGA NCHINI KENYA WAHOFIA KULISHWA NYAMA YA PUNDA


Wakazi wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamekumbwa na hofu ya kuwa huenda wamekuwa wakilishwa nyama ya punda baada ya kuonekana mabaki ya vichwa vya punda katika maeneo kadhaa ya kaunti hiyo.

Mkazi wa kaunti ya Kirinyaga katika kijiji cha Murubara Bi, Wariara Githinji amesema wameshangazwa kubaini vichwa vinne vya punda vikiwa vimetelekezwa katika eneo mabalo wanyama hao wamechinjwa.

Vichwa hivyo na mabaki mengine ya punda ikiwemo utombo vilibanika na watoto waliokuwa wakienda shule ambao walikuwa wakishangaa hali iliyowavuta watu wazima waliokuwa wakipita njia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni