Bw. Ladislaus Matindi akisamilimiana na Gavana wa Anjoun Mhe. Abdou Salam Abdou
Mazungmzo yakiendelea katika ofisi ya Gavana
Mhe Balozi akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Kisiwa
Mhe Balozi akiongoza kikao na wadau wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun
Mke wa Balozi Mama Irene Kilumanga akimsalim Gavana.
Wajumbe walipowasili Kisiwa cha Anjoun
TAARIFA FUPI ZIARA YA UJUMBE WA ATCL VISIWANI KOMORO TAREHE 06 FEBRUARI, 2017
Ujumbe
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL Limited) uliwasili Visiwani
Komoro tarehe 5 February, 2017. Ujumbe huo ukiongozwa na Bw. Emmanuel
Korosso ulipokelewa na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania,
Visiwani Komoro. Aidha Mwenyekiti huyo aliongozana pia na Bw. Ladislaus
E. Matindi Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL.
Madhumini
ya ziara hiyo ilikuwa ni kuja kuangalia namna gani ATCL inaweza kutanua
wigo wa safari zake Visiwani Komoro. Hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa
shirika hilo kuweza kulidhibiti kikamilifu soko la anga la Visiwa vya
Komoro ambapo kwa sasa Soko hilo limekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa
mashirika mengine ya Kimataifa kama vile Ethiopian Airlines, Air Madagscar, Kenya Airways n.k.
Katika
ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kuongozana na Mhe. Balozi kwenda
Kisiwa cha Anjoun na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe.
Abdou Salami Abdou. Ifahamike kwamba Shirika la ndege la ATCL hufanya
safari zake mara tatu kwa wiki Visiwani Komoro ambapo ndege hiyo hutua
katika uwanja wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim Jijini Moroni.
Komoro ni Muungano wa Visiwa Vitatu ambavyo ni Anjoun, Ngazidja na Moheli. Hata
hivyo imeonekana kuwa abiria wengi wanaosafiri kuja Tanzania kwa ajili
ya shughuli za biashara hutokea Katika Kisiwa cha Anjoun. Imejidhihirisha kuwa abiria
kutoka Ksiwa cha Anjoun hupata usumbufu kwa vile hakuna safari za moja
kwa moja kutoka Kisiwa hicho kwenda Dar es Salaam, hali ambayo
imeonekana kuongeza ghara za usafiri kwa abiria hao.
Aidha
katika mazungumzo yao na Gavana wa Kisiwa cha Anjoun ujumbe huo
uliwasilisha maombi ya ATCL kupewa kibali cha kutua Kisiwa cha Anjoun
ambapo Gavana huyo aliridhia maombi hayo na kueleza kufurahishwa kwake
na dhamira ya ATCL kufanya safari zake Kisiwani hapo.
Mhe.
Gavana alieleza pia safari za ATCL Visiwani hapo zitasaidia katika
kukuza mahusiano ya biashara kati ya Tanzania na Komoro pamoja na
kupunguza gharama za usafiri kwa abiria wanaotokea kwenye Kisiwa hicho.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro, Mhe. Chabaka
Kilumanga alieleza pia kuwa jukumu kubwa la Ubalozi ni kuhakikisha kuwa
mahusiano ya biashara kati ya Tanzania yanakuzwa na kwamba usafiri wa
anga ni njia moja wapo ya kukuza mahusiano hayo. Mhe. Balozi aliendelea
kwa kueleza kuwa lengo ni kuona Dar es Salaam inakuwa ni kitovu cha
Biashara hivyo hakuna budi kukawepo ufanisi katika usafiri wa anga na
usafiri wa maji.
Sambamba
na hilo, Ujumbe wa ATCL pamoja na Balozi walipata fursa pia ya kufanya
mazungumzo na wadau kutoka Sekta ya Biashara wa Kisiwa cha Anjoun ambapo
pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Ladislaus
Matindi aliwahakikishia wana Anjouna kuwa shirika la Ndege la ATCL la
sasa sio kama la zamani na kwamba shirika hilo limejidhatiti katika
kuboresha huduma zake.
Aidha
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa shirika hilo limeweza kuondoa usumbufu
mwingi uliokuwa ukijitokeza hapo nyuma ikiwemo suala la upotevu wa
mizigo, kufutwa kwa safari bila maelezo, ucheleweshaji wa abiria na
mizigo yao, alieleza kuwa
shirika hilo linatambua umuhimu wa wadua wa biashara kutoka Kisiwa cha
Anjoun na ndio maana ameeongozana na Mwenyekiti wa Bodi Visiwani hapa
ili kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanya biashara hao na
kushauriana juu ya namna gani changamoto hizo zitapatiwa ufumbuzi.
Kw
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL Bw. Emmanuel Korosso alielekeza
shukurani zange kwa wadau wa biashara Kisiwani Anjoun na kuendelea
kusisitiza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limedhamiria katika
kuboresha ufanisi kwenye utendaji wake na kwamba shirika hilo linasimama
pamoja na Wakomoro katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa.
Mwenyekiti
aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua changamoto ambazo zimekuwa
zikiwakabili abiria wa Anjoun na kwamba changamoto hizo siku zake
zinahesabika. Aliahidi kuwa yale yote ambayo ATCL imedhamiria kufanya
yatatekelezwa tena kwa wakati muafaka kwani Ofisi ya Ubalozi ipo kwa
ajili ya kufanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni