HAKIMU MFAWIDHI MAGU ATOA WITO KWA MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO

Watumishi wa Mahakama wilayani Magu wakiandamana na bango lenye ujumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria

Na Shushu MAGU

HAKIMU mfawidhi wa wilaya ya Magu mkoani mwanza Edmund Kente ametoa agizo kwa mahakimu na watumishi wote wa idara za mahakama kuhakikisha wanawashughulikia wananchi kwa uhakika na ipasavyo.

Wito huo ameutoa katika siku ya maadhimisho ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahaka ya wilaya ya magu chini ya kauli mbiu iliyosema kuwa Umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Kente alitumia wito huo kuwataka mahakimu wote wa mahakama za mwanzo kuweza kubadilika na kufanya kazi kwa weredi ili kuleta ufanisi mkubwa katika kazi zao za kuwahudumia wananchi wa hali ya kawaida kwa kuwawezesha kupata haki zao za msingi.

Aliongeza kuwa wananchi wanapokimbilia mahakani lengo lao ni kupata haki sitahiki ili waweze kuepukana na hicho kilichokuwa kikiwasumbua katika kutambua haki zao lakini hali imekuwa sivyo na matarajio yao nah ii ni kutokana na mahakimu wengi kutokufanya kzi kwa weredi.

Nimeletewa malalamiko mengi na wananchi juu ya kuzungushwa kwa kesi zao na mahakimu bila kuwepo kwa sababu za msingi na kuweza kuyatolea maamuzi magumu kwa baadhi ya mahakimu wanaokuwa na tabia za kuwazungusha wananchi Alisema”.

Aidha hakimu huyo mfawidhi akiongeza kuwa siku mbili nyuma waliweza kufanya ziara akiwa na watumishi wote wa idara ya mahakama katika gereza la magu ili kuwajulia hali wafungwa na kuwapatia zawadi mbalimbali kwa lengo la kutojenga uadui kati yao na vyombo vya haki.

Pia aliongeza kuwa jeshi la polisi na mahakama ni vyombo vinavyotegemewa katika kutenda haki kwa wananchi lakini wengi imekuwa sivyo nah ii ni kutokana na wachache kutozingatia maadili ya kazi zao.


Kwa upande wake hakimu wa Mahakam ya mwanzo wilaya ya magu Reuben Muganyizi amempongeza hakimu kente kwa utendaji wake wa kazi katika wilaya hiyo na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa katika jamii yetu.

Aidha ametumia muda huo kutoa ushauri kwa mahakimu wenzake kwa kuiga tabia za kiongozi wao ambaye amekuwa akitetea wananchi wa chini kwa kuwasiadia sheria mbalimbali zikiwemo za ardhi na nyingine kibao kwa lengo la kuwaweka sawa katika kutambua haki za msingi.

Muganyizi aliongeza kuwa si vyema na wala si sahihi kuwaweka wananchi mahakamani kwa muda mrefu bila kuwapatia huduma wanazohitaji kupata toka kwetu wanasheria ambao tupo kwa ajili ya kuwsaidia wananchi.

Peter Msanja ni mchungaji mstaafu wa kanisa la Mitume ya Yehova alisema Mahakam ni chombo cha kutoa haki katika jamii lakini leo imekuwa ndio chombo cha upotoshaji katika jamii isiyojua sheria lakini tangu tumpate hakimu kente mambo yamekuwa tofauti na awali.

Mchunga huyo aliongeza kuwa hakimu mfawidhi anafanya kazi kwa weredi na kwa haki ndio maana watu wengi uenda kumuona yeye ili aweze kuwahudumia katika kutatua kero zao pasipo upendeleo wa aina yeyote ile.

Rushwa upofusha hivyo watu wasitumie kitu ambacho hata kwenye vitabu vya mungu vimekataliwa kwa makusudi ya kusongesha taifa mbele katika maendeleo”

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni