MKE
 wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
 Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi 
mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo. 
Wake 
wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) 
wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua 
kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao
 ni sehemu ya jamii. 
“Vitabu
 vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa 
umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea 
wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi 
mnahitaji faraja,” amesema. 
Amesema
 wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la 
kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa
 raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya 
tabia. 
“Ni 
siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha 
kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema 
tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua 
mnamahitaji mengi,” amesema. 
Katika
 gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa 
wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave 
aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka, 
tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”. 
  Mke 
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa 
Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na 
mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya 
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa zawadi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa
 Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa 
wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya mahabusu ya 
Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 
14, 2017
PICHA NA IKULU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni