Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amewapiga marufuku
polisi wa Mkoani Arusha kuwasumbua ovyo wafanyabiashara wadogo wa
madini(Brokers) katika maeneo yao yakufanyia biashara bila kufuata utaratibu
maalumu.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga kikao chake na
wafanyabiashara hao katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kikiwa
na lengo lakusikiliza kero zao na kuongeza ushirikiano baina ya wafanyabiashara
hao na serikali yao ya Mkoa wa Arusha.
“Ninamwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuanzia
sasa kusimamisha zoezi hili lakuwasumbua hawa wafanyabiashara wadogo wa madini
katika maeneo yao ya biashara bila kufuata taratibu”.
Aidha Gambo amewaagiza Kamishina wa Mamlaka ya mapato
(TRA) Arusha na ofisi ya madini kanda ya Kansazini kuandaa mpango maalumu
wakutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wa Mkoa wa Arusha juu ya utoaji wa leseni za madini na ulipaji wa kodi.
Alisema hayo baada ya wafanyabiashara hao kutoa malalamiko
yakutoelewa taratibu za upatikanaji wa leseni
za madini na pia hawana elimu tosha juu ya ulipaji kodi kwani wengi wanaona
wanatozwa kodi kubwa ambazo haziendani na hali halisi ya biashara zao
wanazofanya.
Akisisitiza zaidi Kamanda wa polisi Mkoa wa
Arusha,Charles Mkumbo amesema jeshi la polisi la Mkoa wa Arusha litaendelea kudumisha
ulinzi na usalama kwa wananchi wote na mali zao.
Hivyo kawataka wafanyabaishara wadogo wa madini wa Mkoa
wa Arusha kuwa na imani na jeshi lao la polisi kwani litaendelea kuwalinda wao
na malizao na hata kwa wale waliokamatwa nakunyang’anywa madini yao, ofisi yake
itafuatilia iliwanaostaili kurudishiwa watapewa mali zao.
Kamishina wa mamlaka ya mapato Arusha(TRA) bwana,Ambili
Mbaluku amesema ni vizuri wafanyabaishara hao wakajitaidi kulipa kodi kadri ya
mapato yao kwasabau serikali inategemea kodi hizo katika shughuli mbalimbali za
maendeleo ya jamii na wao watajitaidi kutoa elimu zaidi juu ya ulipaji kodi
mzuri.
Pia kamishina wa madini kanda ya Kansazini Adam Juma
amesema nivizuri wafanyabaishara hao wakakata leseni kwaajili yakuendesha
shughuli zao kihalali huku wakitambulika na mamlaka husika kuwa
niwafanyabiashara halali wa madini.
Mkuu wa Mkoa Gambo alimalizia kwakuwaadi kuendelea
kukutana nao mara kwa mara angalau kila baada ya miezi mitatu na wafanyabiashara
hao ilikufanya tathimini ya mambo mbalimbali ambayo wamekubaliana kama yatakuwa
yamefanyiwa kazi na pia kama kutakuwa na mengine yaliyojitokeza.
Pia amewata wafanyabiashara hao wadogo wa madini kukaa
pamoja na kamishina wa madini wa kanda ili
kuchagua uongozi wa mda wa chama chao kwakuwa uongozi uliopo ulionekana
kutokubalika na wanachama walio wengi,
na uongozi huo utakuwa ukishughulikia matatizo na kero za wanachama wake kwa
ukaribu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni