MOROGORO : 66 MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA

Watu 66 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani wa Morogoro kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za madawa ya kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (leo Jumatatu mchana) amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni mwendelezo wa operesheni ya kupambana na dawa za kulevya na matukio mengine ya uhalifu.
Katika msako uliofanywa na jeshi hilo pia gari aina ya Noah imekamatwa ikijihusisha na usafirishaji wa sawa hizo na kukutwa na viroba 39 vya bangi, pamoja na nyara za Sérikali.
HT : MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni